Header Ads Widget

BAWACHA KAGERA WAJIBU KAULI ZA MWENYETI WA UWT TAIFA MERY CHATANDA DHIDI YA MWENYEKITI MBOWE.



Na Theophilida Felician Kagera.


Umoja wa baraza la  wanawake wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema BAWACHA  Mkoa Kagera umekutana  pamoja kwenye kikao  na kuzungumzia mambo kadha wa kadha ya chama  ikiwemo ya kutoa tamko la ufafanuzi  wa  kauli za Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi UWT taifa Mhe Mery Chatanda ambazo amekuwa akizitoa zikimlenga moja kwa moja mwenyekiti wa CHADEMA  Taifa Mhe Freemani Aikaeli Mbowe.



Akifafanua kwa undani  kauli hizo mbele ya wanawake wa BAWACHA  Kagera  kutoka majimbo yote 9 ya #æ amekuwa akitoa kauli  tofauti tofauti dhidi ya Mwenyekiti Freemani Mbowe kupitia njia mbali mbali ikiwemo ya vyombo  vya habari na mikutano ya hadhara.



"Mwenyekiti  wa UWT taifa Mery Chatanda alisikika kwenye vyombo vya habari kadhaa akitoa kauli za kumuataki Mwenyekiti wetu wa chama  Taifa Mhe Mbowe  sasa hatuwezi kukubali kuona Mwenyekiti wetu anaatakiwa sisi kama baraza  tukakaa  kimya haiwezikani" amesema Mwenyekiti Pendo Ngonyani Mbele ya wanawake katika kikao hicho kilichowakutanisha Manispaa ya bukoba



Mwenyekiti huyo ametolea mfano wa kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na kiongozi huyo ni pamoja na kauli alizozitoa kwenye mkutano wa hadhara Mkoani   Lindi tarehe 16 /7/2023  "alitoa kauli  hivi ni  kwamba  mhe Mbowe hana Shukrani  na mnukuu  Mery Chatanda  alisema  Mbowe aliwekwa ndani na Rais Magufuli Rais Samia akamtoa naomba nimkosowe   Mwenyekiti wa UWT Tanzania  ni hivi na mkumbusha aliyemuweka ndani  Mwenyekiti Mbowe  ni Rais Samia nasiyo Rais Magufuli Mwenyekiti wetu alikamatwa Tarehe 20/7 2021 akiwa Mwanza ikiwa ni miezi minne baada kutokea kifo cha Magufuli kwa hiyo suala la kubambikiziwa  kesi ya ugaidi Mwenyekiti wetu halikuwa la Magufuli bali lilikuwa ni  la Rais Samia" ameeleza bayana Pendo Ngonyani.



Kauli nyingine alizozitoa   ambazo zimekuwa zikitolewa na Mwenyekiti wa  UWT dhidi ya Mbowe  ni pamoja na nakusema kuwa Mwenyekiti Mbowe amekuwa  akituhumu kuuzwa kwa bandari ya dar kwenye kampuni ya Dp Waorld.



Ufafanuzi kuhusu suala la bandari kwa pamoja wanawake hao wamebainisha kuwa wanapinga vikali  mkataba wa bandari hiyo kwani una mapungufu kadhaa maana  hauonyeshi ukomo wala  hauonyeshi  watawekeza kiasi gani nataifa litapata kiasi gani.



Hata hivyo Ngonyani amegusia suala la madai ya Katiba mpya jinsi linavyoendelea kufanyiwa kazi  kwa malengo ya kufanikiwa  zaidi  ili kuhakikisha katiba mpya inapatikana kwa wakati na sivinginevyo.



Ameongeza  kusema kuwa  kwa sasa chama cha Chadema Taifa kipo ukanda wa ziwa Victoria  kwa ajili ya shughuli mbalimbali za chama ambapo tarehe 28/7 mwaka huu wa 2023 Viongozi wa chama hicho Taifa watakuwa  Kagera ili kukutana na  wananchi wa Mkoa huo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI