Header Ads Widget

UPINZANI TANGA HALI TETE WANACHAMA 542 KUHAMIA CCM.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga akizindua mashina ya Chama hicho

NA MBARUKU YUSUPH,MATUKIO DAIMA APP TANGA. 

VYAMA vya upinzani Mkoani Tanga vimeendelea kutetereka baada ya wanachama 542 toka vyama hivyo vya upinzani kuhamia Chama cha Mapinduzi(ccm) baada ya Mwenyekiti wa Chama hicho Rajabu Abdurahman kufanya ziara ya kufungua mashina nane ya wakereketwa wa ccm ndani ya Jiji la Tanga. 


Ziara hiyo ya Mwenyekiti huyo aliyeambatana na Viongozi ngazi ya Mkoa,Wilaya na Meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga alisema wakati umefika kwa wananchi wa Mkoa wa Tanga kuunga mkoni jitihada zinazofanywa na chama hicho kwa ajili ya kuleta maendeleo yatakayokuwa na tija kwa kila mwananchi.


Abdurahman alisema hapakukuwa na sababu ya kusimama katika majukwaa na kuanza kutoa lugha za matusi kwa viongozi wa vyama vya Upinzani na badala yake ni kufungua milango kwa atakeona CCM ndio chama sahihi kitakachokuwa sehemu bora ya kukitumikia na kuleta maendeleo Mkoani hapa.


"Wapo waliotubeza kwa lugha mbaya lakini sisi hatukuona sababu ya kuwatusi zaidi ya kukaa nao na kuona namna gani tunaweza kuujenga Mkoa wetu na haya ndio matunda yake"Alisema Rajabu. 


Aidha alisema hivi vyama havipo kwa ajili ya maslahi ya wananchi badala yake vipo kwa ajili ya maslahi ya viongozi wao na ndio maana huwa havina uwezo wa kutatua kero za wananchi badala yake vimejiwekeza kwenye kupambana na Serikali,kubeza kila kinachofanywa na mwisho wake vinasambaratika.


Alisema wananchi wamechoka kudanganywa na wanahitaji Chama ambacho ni sikivu na kitakachokuwa tayari na uwezo wa kusikiliza shida na kero zao na kuzitafutia njia sahihi ya kutatua badala ya kupewa ahadi ambazo hazitekelezeki miaka na miaka.


Mwenyekiti huyo alijibu hoja za baadhi ya viongozi wa mashina aliyoyafungua juu manyanyaso yanayofanywa na baadhi ya Askari Polisi ambao sio waadilifu kwa kukamata pikipiki za vijana wa bodaboda ambazo zipo kwenye maegesho.


Rajab alisema sio sahihi kwa Askari kukamata chombo cha moto ambacho hakipo barabarani kikiendeshwa na kufanya hivyo ni kinyume nataratibu za kazi zao na Askari hao wanayohaki ya kisheria kukamata chombo chochote cha moto kitakachovunja sheria kikiwa kipo barabarani kinatumika.


"Unapokamata pikipiki ikiwa imepaki sawaswa uje nyumbani kwangu uje uikamate gari langu na utalikamataje wakati limekaa labda ni bovu lakini likiwa linaendeshwa Askari wanayohaki wa kulikamata na kulikagua ndio kazi zao"Alisema.


Rajabu alisema kero hizo alishazungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga na kuona njia gani sahihi ya kukabiliana na vitendo vya uvunjifu wa sheria za usalama barabarani vinaweza kudhibitiwa na kuwaonya baadhi ya Askari ambao sio waadilifu wakati wa kutimiza majukumu yao na kusababisha kero kwa wananchi.


Hata hivyo aliwataka wanachi hao waache kuvunja sheria barabarani kwa madai Mwenyekiti huyo atakwenda kuwasaidia pindi watakapotiwa hatiani jambo ambalo halitakuwa rahisi na kufanya hivyo maana yake ni kutetea uvunjifu wa sheria za usalama barabarani ambapo kitendo hicho ni kinyume na sheria za Nchi.


"Bodaboda ni sehemu ya ajira kwa vijana wetu lazima vijana wenyewe wafuate sheria zitakazo wawezesha kufanya kazi zao kwa amani na Askari wetu watimize majukumu yao kwa welding?Alisema Rajabu.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI