NA Dishon Linus
Joash Onyango inaelezwa tayari ameshamalizana na Singida Fountain Gate FC kwa kandarasi ya miaka miwili akitokea Simba SC.
Taarifa zinasema Simba SC wamekubali kumuachia Joash Onyango akatafute changamoto nyingine baada ya kuomba kuondoka kwa muda mrefu kwa kuwaandikia barau Simba SC zaidi ya mara mbili.
Simba SC kwasasa ipo kwenye mpango wa kuongeza Mlinzi mwingine Mzawa kuziba pengo atakaloacha Joash Onyango na kwenda kuungana na Henock Inonga, Kennedy Juma na Che Fondoh Malone.
0 Comments