Header Ads Widget

WAMILIKI WA VYOMBO VYA USAFIRI WA MAJINI WATAKIWA KUVISAJILI

 




Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP DODOMA


SERIKALI Kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imewaonya wamiliki wa vyombo vya usafiri wa majini  vinavyotumika katika shughuli za Uvuvi kuhakikisha vimesajiliwa na kupata Cheti Cha uthibitisho .


Pia amewaonya wavuvi wanaokwepa kutumia Mialo ya Uvuvi iliyosajiliwa na kutumia Mialo Bubu hali hiyo inasababisha kuendelea kutokea kwa vifo holela kwa wavuvi na kukosekana kwa Takwimu sahihi za za Matukio hayo.


Onyo hilo limetolewa Jijini Dodoma na Afisa Mvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Nathanael Mboji wakati Akizungumza na wadau katika sekta ya Uvuvi waluokutana kujadili namna ya kukabiliana na Matukio ya ajali za majini.



Akiongea katika kikao Cha wadau cha kuimarisha juhudi za usalama kwenye maji Mkurungezi Mtendaji wa Shirika la EMEDO Editrudith Lukanga amesema Tanzania imepiga hatua katika usalama wa maji na kuizia kuzama maji kwa kuzindua Mtandao wa kitaifa wa kuzuia kuzama maji (NDPN).


Amesema jumla ya mashirika 26 yamekusanyika na kuanzisha Mtandao wa kitaifa wa kuzuia kuzama maji Kama Jukwaa  mahususi la kuratibu utetezi wa kuzuia vifo vinavyotokana na kuzama nchini kote.


Amesema mpango huo unalengakuunganisha wadau wote nchini ili kushughulikia Suala muhimu la kuzama maji na kufanya kazi kwa pamoja ili kupunguza vifo vya vinavyotokana na maji.



" Kuzama ni moja ya sababu kuu ya vifo vinavyoweza kuzuilika  duniani kote na kuleta athari kwa Watu binafsi ,familia na jamii," Amesema 


Pia Amesema wanakabiliwa na Changamoto ya Takwimu hali inayowafanya kushindwa kuongea Hali ya vifo kwa wavuvi na ndio Maana wamekutana kuwa na iratibu wa pamoja ili kuweza kujua nini kifanyike kuwa na Takwimu na Sera kwa ujumla.




Kwa Upande wake Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa mwanza Mrakibu wa zima moto na uokoaji  Kamila Labani Amebainisha hatua wanazochukua  kuthibiti Matukio ya kuzama katika ziwa Victoria


Amesema wameojiwekea mbinu na mikakati  Maalumu ambapo visiwa vyote 73 vya ziwa Victoria wameanzisha marafiki wa zimamoto.


" Hata kwenye kanuni yetu ya utendaji kazi inatutaka kuanzisha vikosi vya kiraia ambapo kwenye kila kisiwa lazima kuwepo na watu watano watakaofundishwa bure mafunzo ya kujiokoa majini," amesema Kamanda huyo.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI