Header Ads Widget

" MABORESHO YANAYOENDELEA KWENYE BANDARI YA DAR ES SALAAM NI UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM"_ MWAKIBETE

 


Na Ibrahim Kunoga,Tanga.


Naibu waziri wa  ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete amesema maboresho yanayoendelea sasa hivi kwenye bandari ya Dar es Salaam ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi CCM mkataba ambao umetaja maboresho ya bandari kwenye bahari ya hindi na maziwa mara 119.


Mwakibete ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na maelfu ya wakazi wa Mkoa Tanga wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Komred Daniel Chongolo uliofanyika Wilayani Korogwe Mkoani Tanga. 


Mwakibete ambaye alitolea mfano bandari ya Tanga alisema serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 400 ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi na kwamba kinachoendelea kwenye bandari ya Daresalaam ni maboresho yanayolenga kuongeza ufanisi na hatimaye bandari hiyo kuwa na mchango mkubwa kwenye pato la Taifa. 


Mwakibete amewaondoa hofu watanzania dhidi ya uwekezaji huo na kuweka bayana uvumi uliopo kwamba mpango huo unazihusisha bandari zote zilizopo kwenye bahari ya hindi na maziwa na badala yake kueleza kwasasa mpango huo upo kwenye baadhi ya gati kwenye bandari ya Daresalaam. 


 "Hakuna bandari yeyote inayouzwa isipokuwa ni mpango wa kuongeza uwezo wa kuhudumia shehena za mizigo zinazoingia na zinazotoka kwenye bandari zetu wanaoleta propaganda kwamba bandari zote maziwa yote huo ni uongo wapuuzeni, "


Akizungumzia uwekezaji wa DP World nchini ambayo inatarajiwa kuwekeza kwenye bandari ya Daresalaam Mwakibete amesema kampuni hiyo inamiliki meli zisizopungua 400 na kwamba inafanya kazi duniani katika nchi 30 na katika bara la Afrika inafanya kazi katika nchi 6.


"Ikumbukwe kwamba ndugu zetu sisi wanatanga sisi hapa tuko jirani na marafiki zetu Kenya ambapo kuna bandari ya Mombasa na Lamu maana yake ni washindani wetu ili mizigo ije kwenye bandari yetu ya Tanga, Daresalaam lazima tutafute ufanisi wenye tija na wamiliki wa meli wasione gharama kuleta mizigo yao kwenye bandari zetu za Tanzania, "alisisitiza, Mwakibete. 


Aliongeza kuwa na wakati mwingine wale wote ambao wamepata nafasi ya kufika bandari yetu ya Daresalaam ukiangalia ng'ambo utakuta kuna meli nyingi na wakati mwingine zinakaa meli 10 - 20 zikisibiri zitie nanga kwenye bandari yetu ya Dar lakini zinashindwa kutia nanga kushusha mzigo lakini ni kwasababu kwenye gati zetu za Daresalaam kwanza ni chache kwasababu sisi tuna magati 12 pekee kwenye bandari yetu ya Dareslaaam wenzetu wa Kenya wana magati 22 wametuzidi magati 10 ndio maana meli nyingi kwahiyo meli nyingi zinakuwa kwenye kina kitegu pale Daresalaam kwasabbu magati yetu ni machache pili hatuna vifaa vya teknolojia vya kushusha kwa wakati na hatuna mifumo inayosomana ili iwe rahisi kwa watu kulipa kodi lakini iwe rahisi meli zikifika ziweze kushusha kwa wakati mmoja. 


Mwakibete amesema madhara yake ni kwamba kadri meli zinavyokaa pale nangani kwa muda mrefu kunakuwa na ulipaji wa gaharama za meli na kwa siku moja ni dola za kimarekani elfu 25 sawasawa na fedha za kitanzania shilingi milioni 58 kwakila siku moja. 


Alisema gharama hizo meli ikikaa siku 10 maana yake ni zaidi ya milioni 58 kwa mara 10 sawa na milioni 580 zinatakiwa kulipwa na yule anayelipa hawezi kulipa na kwamba yule ambaue amekodi meli gharama atakayolipa itatokana na wale wenye mizigo ndani ya meli madhara ambayo yanaonekana kumuathiri mwananchi. 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI