Header Ads Widget

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA BUNDA HAINA HUDUMA YA MAJI TAKA

 



 Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


MAMLAKA ya majisafi na usafi wa mazingira Bunda (BUWSSA)haina huduma ya majitaka,hivyo magari ya watu binafsi ambayo yanasimamiwa na Halmashauri ya mji wa Bunda ndiyo yanatumika katika kutoa huduma za majitaka. 


Hayo yamebainishwa jana jijini Dodoma na Mkurungezi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Esther Gilyoma wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu utendaji kazi na muelekeowa Taasisi huyo ya Bu


Hivyo kupitia Mamlaka ya maji Bunda kwa mwaka wa fedha 2023/2024 tunategemea kuanza kujenga miundo mbinu ya majitaka eneo la Butakale liliyoko Mjini Bunda.  


Kuhusu uzalishaji maji Mkurungezi Mtendaji huyo amesema Mamlaka hiyo ina uwezo wa kuzalisha maji kutoka kwenye chanzo kipya na cha zamani lita za ujazo 15,264,000 kwa siku ambayo hayajatibiwa na ambayo yametibiwa ni lita za ujazo 10,320,000 kwa siku kutoka kwenye chanzo ambacho kimekamilika mwaka 2023.


Amesema Mamlaka ina uwezo wa kuzalisha wastani wa lita 3,870,000 kwa siku kutokana na ufinyu wa mtandao wa bomba kutofika maeneo yote ya Mjini Bunda, hivyo Mamlaka ina akiba ya maji ya kutosha ya lita za ujazo 6,450,000 yaliyotibiwa na lita za ujazo 4,464,000 kupitia chanzo cha zamani ambazo zinaweza kuwafikia wanachi kwa 95% kufikia mwaka 2025. 


"Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda imeweka mikakati ya kupunguza upotevu wa maji ulioandaliwa ikiwa ni mpango mkakati wa kupunguza upotevu wa maji wa miaka mitatu ulioanza mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2023/2024 unaoendana na mpango wa kibiashara wa Mamlaka ya maji," 


Na kuongeza "Hivyo  Mamlaka hiyo imeandaa andiko la mradi kwa ajili ya kukopa fedha kiasi cha shilingi 815,000,0000 kutoka Mfuko wa Maji ili kuhakikisha upotevu wa maji unapungua kuanzia mwaka wa fedha 2023/2024," Amesema Mkurungezi huyo


Amebainisha kuwa Kupitia Mamlaka hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024, inategemea kuanza kujenga miundo mbinu ya majitaka eneo la Butakale lililopo Mjini Bunda. 


Ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023, Mamlaka hiyo ina jumla ya wateja 7,556 ambapo kati yao kuna wateja wa nyumbani,Taasisi na Biashara.


Miradi inayoendelea ya ujenzi wa upanuzi wa mtandao wa bomba mjini Bunda kwa mwaka wa fedha 2022/23 itakapokamilika, Mamlaka hiyo itaweza kufikia asilimia 91 ya wananchi wanaopata huduma ya majisafi Mjini Bunda.


Aidha Amesema Kwa mwaka wa fedha 2023/24, Mamlaka imetenga jumla ya shilingi 12,705,000,000 ambapo miradi iliyopendekezwa ikijengwa kwa mwaka huo wa fedha, Mamlaka itaweza kufikisha huduma ya maji kwa asilimia 95 kufikia mwaka 2025.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI