Header Ads Widget

JKT YAWEKA MIKAKATI KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO YA CHAKULA NCHINI

 


NA HAMIDA RAMADHAN MATUKIO DAIMA APP DODOMA


MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, amesema katika kutekeleza azma ya Rais Samia Suluhu Hassan ya Tanzania kuwa kapu la chakula katika bara la Afrika wameweka mikakati mbalimbali ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula.


Meja Jenerali Mabele, amesema hayo leo Julai 27,2023 jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya JKT na mwelekeo wake katika mwaka wa fedha 2023/2024.


Amesema katika mwaka huu wa fedha kiasi cha Sh. biloni nne kimetengwa kwa ajili ya kujenga miundombinu ya umwagiliaji ili kuongeza maeneo ya kilimo na uzalishaji ili kukidhi hitajhio la chakula kwa vijana na usalama wa chakula kwa taifa.


Hivi sasa tunazungumza na wizara ya Kilimo kuona ni kwa jinsi gani ule mradi wa Jenga kesho iliyo bora (BBT), kuunganishwa na vijana wanaohitimu mafunzo ya JKT ili kuwasaidia kupata shughuli za kufanya pindi wanapomaliza mikata yao ya miaka miwili na kukosa nafasi ya kuajiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama nchini”amesema


Aidha, ametoa wito kwa vijana nchini kuchangamkia fursa za mafunzo zinazotolewa na jeshi hilo ili kujipatia ujuzi wanaoweza kuutumia mara watakapo maliza mkataba wao wa miaka miwili ya kulitumikia Jeshi hilo.


Kadhalika Amesema wako tayari kupokea waandishi wa habari ambao watahitaji kujiunga na mafunzo yanayotolewa katika kambi zao mbalimbali nchini ili kuwajengea uzalendo.


Hata hivyo, Mkuu huyo amesema Jeshi hilo la JKT lipo tayari kupokea waandishi wote nchini ambao watahitaji kujiunga mafunzo ambayo yanatolewa kwenye kambi mbalimbali nchini ili kuwapatia fursa ya kujifunza vitu mbalimbali ambavyo vitawajenga kuwa wazalendo wa nchi yao.


“Mimi nipo tayari kuwaandalia programu nzuri ya mafunzo wanahabari wote nchini ambao watakuwa tayari kujiunga na mafunzo yanayotolewa na Jeshi hili katika kambi zetu mbalimbali mikiwa tayari tunawakaribisha sana”amesema Meja Jenerali Mabele


Aidha, amesema katika mwaka huu wa fedha JKT, imetengewa kiasi cha Sh. biloni 9.96 kwa ajili ya kujenga miundombinu na kuongeza kambi zingine kwa ajili ya kuongeza idadi ya vijana wanaopatiwa mafunzo kwa mujibu wa sheria, wale wa mkataba pamoja na wale wa mafunzo ya hiyali.



kwa Upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amelipongeza jeshi hilo kwa namna linavyotoa mafunzo ya uzalendo kwa vijana na makundi mengine nchini.


“Meja Jenerali Mabele, niwapongeze kwa kazi nzuri manayoifannya na mimi nitazungumza na vyama vya waandishi wa habari nchini kuona ni kwa namna gani tunaweza kuwapeleka JKT waandishi wetu waje wajifunze ili kuwa wazalendo watakapotoka huko hata karimu zao zitakuwa na uzalendo mwingi na taifa lao”alisema Msigwa




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI