Na,Jusline Marco:Arusha
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Mhe.Innocent Bashungwa amesema kuwa Wizara kwa kushirikiana kwa karibu na TPDF itahakikisha kwamba CSC – Duluti inaendelea kujitahidi kuwa moja ya vyuo bora vya Ukamanda na Utumishi.
Mhe.Bashungwa ameyasema hayo wakati akihitimisha mafunzo ya kozi ya Ukamanda na Unadhimu kundi la 37 /22-23 maafali yaliyofanyika katika Chuo cha Ukamanda na Unadhimu CSC kilichopo Duluti -Tengeru Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.
Aidha amewataka wahitimu hao kutambua kuwa Kozi ya Ukamanda itawapa maarifa na ujuzi unaohitajika, ili kutekeleza majukumu yao kwa weledi pamoja na kuwapa msingi wa kiakili katika masomo zaidi na kuleta mabadiliko makubwa kwenye nchi zenu.
Ameongeza kuwa wahitimu hao wana mchango mkubwa katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwenye kurejesha demokrasia na ulinzi wa amani barani Afrika na duniani kwa ujumla.
Amezipongeza nchi ambazo zimetoa wananjeshi wao kushiriki kozi katika chuo hicho ambapo ameomba ushirikiano na uhusuano uliopo uendelee kudumu na Hata hivyo jumla ya wahitimu 65 wa hadhi ya PSC kutoka katika nchi 11 ambazo ni Jamhuri ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Jamhuri ya Kenya, Ufalme wa Eswatini, Jamhuri ya Malawi, Jamhuri ya Msumbiji, Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria, Jamhuri ya Rwanda,pJamhuri ya Afrika Kusini na Jamhuri ya Uganda wamekabidhiwa vyeti vya kuhitimu kuhitimu kozi yao.
Ameongeza kwa kuwataka kuwa mabalozi wazuri na wenye nia njema,huku akisema kwamba wahitimu wa kike ni sehemu muhimu ya jumuiya ya kijeshi.
Naye Mkuu wa Chuo hicho Brigedia Jenerali Sylvester Damian Ghuliku katika hafla hiyo amesema kuwa chuo kinajivunia maarifa yaliyotolewa kwa maafisa wakuu kutoka ndani na nje ya nchi.
0 Comments