Na,Jusline Marco;Arusha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini zote nchini kuongeza juhudi katika kutoa mafunzo ya dini na nyumba za ibadi zitumike kuwa ni maeneo ya kujenga maadili ya watanzania dhidi ya maovu na kuondoa mmomonyoko wa maadili uliopo sasa.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 40 ya Chuo cha Biblia Sakila kilichopo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha ambapo amesema viongozi wa dini na wa umma wanao wajibu mahususi wa kuilea jamii kwa kutoa mafundisho sahihi na endelevu ya dini ili kuiwezesha na kutambua kufuata yote yaliyo mema kama ambavyo amri za Mungu zisemavyo na kuacha mabaya ambayo ni chukizo kwa Mwenyenzi Mungu.
Amesema ni vyema viongozi wa dini kutumia vizuri huduma za kiroho na ibada kujenga jamii yenye tabia njema,utii pamoja na kuheshimu mamlaka zilizopo huku wakiwafundisha vijana kuwa raia wema na wazalendo na wenye manufaa kwa nchi hali itakayopeleke kuwepo kw viongozi wacha Mungu wanaojitoa katika kuhudumia watanzania wenzao katika uadilifu na wasiokula rushwa.
Sambamba na hayo Majaliwa amesema kuwa moja ya majukumu ya taasisi za dini ni kutoa mafunzo ya kiroho yanayoifanya jamii kuwa na hofu ya mwenyezi Mungu ambapo katika majukumu hayo amezitaka taasisi hizo kukabiliana na mmomonyoko wa maadili kwa kuibadilisha jamii inayowazunguka kutoka katika tabia ovu kwenda tabia iliyo njema ili kuwawezesha wananchi kuishi kwa amani.
Ameeleza kuwa katika kipindi hiki yamekuweoo matukio mbalimbali ya mmomonyoko wa maadili kwa rika zote na kuongezeka kwa vitendo viovu ikiwemo mauaji,ubakaji ,ulawiti,ushoga na usagaji,uvaaji wa mavazi yasiyo na staha pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya ambapo amesma vitendo hivyo havikubaliki katika jamii hususani ya kitanzania.
"Maaskofu,wainjilisti,wachungaji na mashekhe kuwa katika nafasi hizo hamjaingia kwa bahati mbaya ,muwe wa kwanza kukemea haya kwani taasisi zenu ndizo zimebeba dhamana ya kuisaidia serikali katika kuielimisha jamii kutambua umuhimu wa amani,utulivu na mshikamano ndani ya tanzania."Alisema Waziri Mkuu Majaliwa
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali ina dhamira ya kubadilisha matumizi ya mifumo ya nishati ya kupikia kutoka kuni na mkaa kwenda kwene mkaa mbadala au nishati ya gesi ambapo amizitaka taasisi zinazotoa huduma ikiwemo shule,vyuo na hospitali kufunga mifumo ya nishati ya gesi kwa ajili ya matumizi ya kupikia.
Aidha amesema ni vyena taasisi zenye watu zaidi ya 10 kuanza kutumia mifumo hiyo ili kuwa wa kwanza katika mabadiliko hayo huku serikali ikijiandaa kuja kutoa tamko la kuachana na mfumo huo na kuvitaka vyuo vinavyotoa huduma kwa jamii kuendelea kuongeza wigo katika utoaji wa elimu kwa kuwekeza kwa wananchi na jamii kama sehemu ya mafanikio yake,huku akiwasisitiza wananchi wanaozunguka taasisi hizo kuona namna bora ya kushirikiana kwa kuzisaidia kulinda rasilimali zao.
Pia ameongeza kwa kuwataka wananchi kutokukubali mtu mmoja au kundi la watu likawatoa kwenye amani na kuwapeleka kwenye magomvi na kusema kuwa amani ikitoweka watakaopata shida ni wanawake na watoto hivyo ni jukumu la kila mmoja kuendelea amani iliyopo na kuungana kwa pamoja.
Kwa upande wake Mkurungezi Mkuu wa Chuo hicho Askofu Eliud Isangya amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungank wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mahusiano mazuri ya vyama vya siasa,jambo ambalo linaonyesha ushirikiano wa kiutendaji katika jamii ambapo amesema kuwa kayika miaka 40 ya chuo amekuwa akitoa elimu ya biblia na mahitaji mengine ya kijamii bure.
Awali akisoma histori ya huduma ya Kituo cha International Evangelism, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maridhiano Tanzania Askofu Israel Maasa amesema tangu kuanza kwa huduma hiyo hadi sasa kumekuwa na mafanikio mbalimbali ikiwemo ununuzi wa gari la kuchimba maji,ujenzi wa zahanati,ujenzi wa chuo cha ufundi maji ya chai,uwepo wa shule ya msingi Sluys Anderson na shule ya sekondari Hebron, eneo la kilima vyakula na kupanua mipaka ya huduma nje ya nchi.
Askofu Maasa amesema pamoja na mafanikio hayo amesema kuanzishwa kwa huduma hiyo pia kumewezesha kufunguliwa kwa matawi katika nchi za Kenya,DRC Congo,Marekani,Afrika Kusini na Rwanda hiku katika upande wa kijamii wakifanikiwa kuwa na kituo cha watoto yatima cha Christ Hope,kituo cha redio cha New life radio network,kugawa viti vya magurudumu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa viungo katika maeneo ya Rukwa,Dodoma,Morogoro,Kilimanjaro,Arusha ba Dar es salaam.
Pamoja na mafanikio hayo pia huduma hiyo imekabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upinzani kutoka kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali,mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali za kuendesha chuo,ambapo pia huduma hiyo ina mipango ya kununua ndege aina ya Jet kwa ajili ya kufanya wepesi wa kufika sehemu mbalimbali za kihuduma pamoja na kupanua wigo wa elimu ya chuo cha biblia kwa level ya P.H.D .
0 Comments