Na Gift Mongi MATUKIO DAIMA App DODOMA
Huenda siku ya leo ikawa ya kipekee kwa viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM)kutoka wilaya ya Moshi Vijijini baada ya kulakiwa na wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Viongozi hawa ambao pia wapo wajumbe wa kamati ya siasa wamelakiwa bungeni hapa mapema hii leo june 20 kufuatia mualiko wa mbunge wa Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi.
Viongozi hao wakiwa na bashasha na shauku kubwa wamefanikiwa kujionea shughuli za bunge zinavyoendeshwa lakini pia kubadilishana uzoefu na baadhi ya wabunge
'Kipekee tumshukuru mbunge Prof Ndakidemi kwa mualiko huu tumejifunza mengi sana lakini pia kuona jinsi bunge linavyoendeshwa'anasema mmoja wa mjumbe kutoka jumuiya ya wanawake.
Miongoni mwa wageni waliokuja kuwasalimu viongozi wa CCM kutoka Moshi vijijini ni pamoja na Mama Salma Kikwete, Dr. Bashiru Ally ,
Pia wakiwemo Mh Waziri Prof Adolf Mkenda, Mh Prof Shukrrani Manya, Mh Prof Palamagamba Kabudi na pia naibu waziri TAMISEMI Deo Ndejebi.
Waliohitimisha zoezi hili adimu ni naibu waziri ujenzi na uchukuzi Eng Geofrey Kasekenya mbunge wa Kiteto mkoani Manyara Edward Olekaita na naibu waziri Ummy Nderiananga,
'Nashukuru kwa kujitokeza unamwona mbungewa viti maalum Kilimanjaro Shally Raymond,mbunge wa viti maalum Ester Maleko,lakini wapo wabunge kama Saashisha Mafuwe wa kule Hai na Priscus Tarimo wa Moshi mjini hakika huu ni upendo.wa.aina yake'anasema Prof Ndakidemi
Jonas Mallya mkazi wa Kibosho Kirima anasema viongozi wa chama kupokelewa kwa heshima inadhihirisha utendaji wao na kuwa ni mwanzo mpya katika utendaji wao wa kazi wa kila siku.
0 Comments