Header Ads Widget

JAJI MKUU ATOA NENO KWA WAKUU WA MIKOA,WAKUU WA WILAYA

 



Na Fadhili Abdallah,Kigoma



JAJI Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma amewataka wakuu wa mikoa na wilaya nchini kujua muundo na utendaji wa mahakama nchini ili kusaidia kukabili changamoto zinazojitokeza katika mchakato mzima wa kusimamia na kutoa haki wa mahakama.


Jaji Mkuu amesema hayo mkoani Kigoma akifungua mkutano wa Tume ya utumishi ya mahakama na kamati za maadili za mahakama na kubainisha kuwa viongozi hao wana nafasi kubwa katika kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika utoaji haki.


Katika hilo Profesa Juma amesema kuwa ukosefu wa mahakama katika baadhi ya wilaya nchini unachangia kuchelewesha utoaji haki katika mahakama nchini hivyo wakuu wa mikoa na wilaya wanazo nafasi kubwa ya kuzungumzia jambo hilo kwa mamlaka mbalimbali na kusimamia utekelezaji wake.



Aidha Jaji alitolea  mfano pia  wa ukosefu wa mkongo wa Taifa katika baadhi ya wilaya na sekta ya Mahakama ambapo ukosefu huo unafanya utekelezaji wa mpango wa uendeshaji wa kesi kwa njia ya video almaarufu  mahakama mtandao.


"Ukosefu wa magereza unaukabili pia mkoa Kigoma ambapo wilaya ya Uvinza inatumia gereza la Bangwe mjini Kigoma na wilaya Buhigwe inatumia gereza la wilaya Kasulu hivyo kuwepo kwa uchelewashaji katika kusimamia na kutoa haki,"Alisema Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma.



Awali akitoa taarifa kuhusu hali ya utekelezaji wa majukumu ya kamati za maadili za mkoa na wilaya Katibu Tawala wa mkoa Kigoma ambaye ni Katibu wa Tume ya maadili ya mahakama mkoa Kigoma alisema kuwa mahakimu wa mahakama za mwanzo, wilaya na mkoa wanazingatia maadili kwa kiasi kikubwa hali inayofanya utoaji haki kuwa wa haki.


Msovela alisema kuwa pamoja na hayo ametaka kupunguzwa kwa vikao vya kisheria vya kamati hizo kutoka vinne kwa mwaka na kubaki viwili kutokana na ufinyu wa bajeti uliopo katika kusimamia vikao hivyo.



Akitoa mafunzo kwa kamati hizo kuhusu muundo, majukumu na mamlaka ya tume ya utumishi wa mahakama na kamati hizo za maadili Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa, Ilvin Mugeta amezitaka kamati hizo zisiishie kutoka adhabu inapotokea ukiukwaji wa maadili kwa mahakimu.


Jaji Mugeta alisema kuwa ni vizuri kuwalea na kufanya vikao nao kabla ya hali hiyo ili kusaidia kuwa na watendaji hao kutokana na changamoto kubwa ya watendaji waliopo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI