Na Gift Mongi MATUKIO DAIMA App DODOMA.
Huenda viongozi walio wengi hawajui dhana mzima ya uendeshwaji wa bunge na majukumu yake kiujumla.
Hii ina maana kwamba wapo ambao wamekuwa wakiona bunge kama tu sehemu ya vikao vya kawaida bila kujua umuhimu wake
Mathalani kwa mfano bado viongozi wa ngazi ya chini hawana uelewa juu ya uendeshwaji wa chombo hicho muhimu
Sasa hapa imepelekea baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM)kutoka halmashauri ya wilaya ya Moshi kufikia bungeni kujionea namna chombo hicho kinavyoendeshwa.
Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro Prof Patrick Ndakidemi ndiye alikuwa mgeni rasmi katika kuwapokea viongozi hao wakiwemo wajumbe wa kamati ya siasa wilaya.
'Karibuni,karibuni,karibuni hapa ndipo mliponituma kwa niaba ya wakazi wa Moshi Vijijini naomba tushirikiane na nina amani mjue kinachoendelea hapa'anasema
Prof Ndakidemi anasema lengo la kuwakaribisha viongozi hao ni kuwaonesha namna shughuli za bunge zinavyoendeshwa
Jonathan Kikumbo mkazi wa Moshi anasema viongozi hao ni jambo jema kujengewa uelewa namna bunge lina yoendeshwa na huenda ikawa na tija katika kuwaongoza wananchi.
'Nimefurahi sana nimeona viongozi wetu wakijengewa uwezo hii ni njia sahihi watakaporudi kwetu huku ngazi za chini'_ anasema
0 Comments