Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
MGOGORO mkubwa uliopo ndani ya chama walimu Tanzania CWT ambao unaendelea umekuwa ukisababishwa na katibu mkuu wa Cha hicho Japhet Maganga ambae amekuwa haeshimu taratibu za uendeshaji wa chama na miongozo ya chama bali hutumia utashi binafsi.
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu CWT Mwal Joseph Misalaba alipokuwa Akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya ukiukwaji wa Katiba ya Chama hicho CWT uliofanywa na Rais wa Chama hicho Leah Ulaya na Katibu mkuu Japhet Maganga
"HII inadhihirika pale ambapo yapo mambo mengi ambayo Kamati ya Utendaji Taifa (CWT) wameazimia kwenye vikao, wameshauriana Kwenye Kundi sogozi (Whatsapp), wamemshauri wakiwa mmoja mmoja lakini amekuwa akikaidi kwa kutumia nafasi yake ya ukatibu Mkuu na kutumia njia haramu kuzuia mawazo mbadala kufika katika vikao vya chama," Amesema Mwal Misalaba.
Aidha Amesema baadhi ya hoja ambapo KUT wamekuwa wakizilalamikia ni pamoja na Katibu Mkuu kupoka Mamlaka ya KUT ikiwamo Kuajiri, Kupandisha Vyeo na Kushusha Vyeo kama Kanuni za Utumishi za Chama za mwaka 2001 na marekebisho ya Mwaka 2011 yanavyosema.
"Tumekuja mbele yenu kutoa ufafanuzi kwa niaba ya viogozi wenzetu ambao inasemekana tumechukuliwa hatua za kinidhamu na Baraza hilo la CWT ambalo ni batili na limetoa maamuzi batili," Amesema .
Na kuongeza "Tunafanya hivi kwa kuwa ni haki yetu kikatiba na kwa kuwa tunapata simu na jumbe nyingi kutoka kwa waliotuchagua, ndugu jamaa na marafiki wakihitaji ufafanuzi kutoka kwetu," amesema Mwal Misalaba
Akisema Kuvunja katiba ya CWT ibara ya III kifungu Cha 22.3 (a) kinavyosema kuwa kazi ya KUT ni Kuendesha na Kusimamia Shughuli za chama. Kufanya hamisho zisizo na tija na zisizozingatia bajeti, hali ya kimaeneo na bila Kushauriana na yoyote.
Chama kuwa na ishara ya mahusiano yasiyoridhisha na serikali kitaifa na Matumizi mabaya ya Madaraka.
Mfano:" Kitendo alichofanya katibu Mkuu CWT siku ya tarehe 06/06/2023 ya kufunga mageti kwa mamlaka yake ni utovu wa nidhamu kwa waliomuajiri (Walimu) na kiongozi Kuendekeza vinyongo na visasi dhidi ya Kiongozi yoyote ambae anahisi hamuungi mkono au hakumuunga mkono hapo awali na kutoa huduma za chama kwa ubaguzi," amesema
Amesema licha ya kuwa tumekuwa na jitihada kadhaa za kutatua migogoro hiyo bali sio Rais wa CWT, Madame Leah Ulaya wala Katibu Mkuu Ndugu Japhet Maganga wamejigusa kutatua mgogoro huo kwa kutafuta majibu ya hoja za wajumbe hao 18 kati ya 32 (zaidi ya asilimia 60 ya wajumbe) wanaosemekana kufukuzwa bali wao wamekimbilia kuita Baraza batili ambalo hata halikufuata hatua stahiki ili kujificha kwenye kichaka.
"Ni imani yetu sisi ni sauti ya wasio na sauti ndani ya CWT yaani walimu na lengo la viongozi hao sio jema kwa chama ndio maana kila jambo wanalohojiwa hukimbilia kuwavua madaraka viongozi wanaohoji na kukusudia kuwavua uanachama," alisema Mwal Misalaba.
Hata hivyo ametaja Maeneo mbalimbali ambayo yamekiukwa na Katibu Mkuu CWT kwenye Katiba, Kanuni na Miongozo mbalimbali. i) Katibu Mkuu amevunja kanuni za CWT toleo la nne la mwaka 2015, kifungu cha 32 juu ya ‘UTATUZI WA MIGOGORO NA NIDHAMU KWA VIONGOZI’ kwa kukikimbia kikao cha KUT na kuliita baraza batili na kukitia chama hasara kwa mgogoro ambao ungemalizwa kwa kukaa pande mbili(UK. 36)ii) Kuvunja katiba ya chama cha walimu Tanzania CWT ibara ya III, kifungu Cha 22.3 (f) kwa yeye kuandaa ajenda ya baraza la Taifa badala ya KUT na hapa ametumia madaraka vibaya.iii) Amekaidi melekezo kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ya tarehe 15/06/2023 yenye Kumb Na.
DA 27/380/12/94 yenye kichwa ‘Utekelezaji wa Majukumu ya Chama kwa Kuzingatia Katiba na Kanuni za CWT’. Barua hiyo ilibatilisha baraza la tarehe 18/06/2023 kwa kuwa liliitishwa bila kupangwa na KUT na kimepangwa kinyume cha utaratibu.
Aidha amesema Barua hiyo pia iliwataka watendaji wakuu wa CWT na wajumbe wa KUT (wanne tuliofikisha malalamiko kwa niaba ya wenzetu) kukutana katika ukumbi wa OSHA mnamo tarehe 16 Juni, 2023 saa tano kamili asubuhi, katika kikao kilichoitishwa na OWM – KVAU bado Katibu Mkuu Ndg, Japhet Maganga alikaidi kuhudhuria kikao hicho kilichokuwa na lengo jema la kutanzua mgogoro huo.iv) Kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 13 (6) (a) pamoja na katiba ya CWT, toleo la sita la mwaka 2014 na kanuni zake kwa kuwanyima wa wanaosemekana ni watuhumiwa kuwapa fursa ya kuwasililiza.
"Tunawapa pole walimu, wanachama wa CWT, viongozi mbalimbali wa chama na serikali, ndugu, jamaa na marafiki na ambao wameumizwa kwa kitendo kilichofanywa na Rais wa CWT na Katibu Mkuu CWT; kuikanyaga katiba ya CWT na kanuni zake kwa kujificha kwenye kichaka cha maelekezo kutoka ofisi flani kumbe ni nutashi wao binafsi,".
Na kuongeza "Bali kipekee tunaiomba serikali yetu sikivu chini ya Rais wetu kipenzi Mama Samia Suluhu Hassan iuchukulie kwa jicho la tatu mgogoro huu ambao unaendelea kuitafuna CWT, kuharibu utulivu wa walimu na viongozi nchini, unaendelea kuleta taharuki na una mlengo wa kuharibu ufanisi wa elimu nchini.
Kwa Upande wake Kaimu muweka Hazina CWT Taifa Mwal Protas Magesa Amesema tangu Rais huyo Leah Ulaya ashike nafasi yake amekuwa ni miongozo wa kuanzisha migogoro.
Pia Rais huyo na Katibu mkuu wamekuwa wakifanya kazi kwa matakwa yao na kutumia mabavu pale unapowaelekeza .
0 Comments