NA HAMIDA RAMADHAN MATUKIO DAIMA APP DODOMA
WAZIRI Wa Kilimo Hussein Bashe amezindua rasmi usajili kwa ajili ya washiriki wa kongamano la usalama wa Chakula litakalifanyika Septemba 4 Hadi 8 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Akiongea hivi karibuni jijini Dodoma Waziri huyo amesema kongamano hilo litaangazia nafasi ya bara la Afrika katika Matumizi ya mbinu bunifu zitakazohakikisha dunia inakuwa na usalama wa Chakula.
Aidha katika uzinduzi huo Waziri Bashe amewaalika wadau wa kilimo wakiwemo wataalamu wa masuala ya mifumo ya Chakula duniani.
Waziri Bashe amesisitiza umuhimu na nafasi ya viongozi wa Afrika katika kuchangia uwepo wa usalama wa Chakula kwa ngazi ya Taifa na bara huku akisisitiza ushiriki wa vijana na Wanawake.
"Wakati tukiendelea na jitihada za kuliwezesha bara la Afrika kuwa kituvu Cha usalama wa Chakula duniani,tunapaswa kuwapa Kipaumbele vijana na Wanawake katika harakati hizi kwa kutumia uwezo wao wa ubunifu na ufanyaji kazi unaoweza kuchangia Maendeleo na uhakika wa Upatikanaji wa Chakula na usalama," Amesema Waziri Bashe.
Amesema kuwa mkutano wa AGRF mwaka huu unafungua milango ya Matumizi ya ubunifu katika kuimarisha kilimo Pamoja na Kufungua milango ya uwekezaji zaidi itakayohakikisha uwepo wa ubunifu utungwaji wa sera bora Pamoja na uwekezaji kwenye sekta ya kilimo.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa hilo Amath Pathe Send Amebainisha kuwa ubunifu sera bora uwekezaji wa kimkakati ni njia sahihi katika kuhakikisha Upatikanaji wa mifumo imara Chakula.
"AGRF 2023 inatuhusisha programu mbalimbali kati ya wadau ambapo watapata wasaha wa kujadiliana na kubadilishana uzoefu ubunifu mbinu mbalimbali wanazotumia katika kutekeleza shughuli za kilimo.
0 Comments