Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 kukagua Miradi 99 yenye thamani ya Shilingi Trilioni 4.4 Pwani
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakati akiwa Halmashauri ya Chalinze eneo la Ubena zomozi tarehe 15 Mei,2023 wakati akipokea Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 kutoka kwa Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Fatma Mwasa.
Amesema Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani hapo utakimbizwa katika Wilaya Saba na Halmshauri 9 za Mkoa wa Pwani umbali wa Kilometa 1,201.95. Ameeleza Mwenge huo utazindua, Kuweka mawe ya Msingi, kukagua na Kufungua miradi yenye thamani ya Shilingi Trilioni 4.4.
Kunenge amesema miradi hiyo ni matokeo ya Uongozi Mzuri wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.
0 Comments