Header Ads Widget

TMDA YATEKETEZA DAWA NA VIFAA TIBA VYA ZAIDI YA MIL. 300 LINDI

 


Na HADIJA OMARY _LINDI....


MAMLAKA ya Dawa na vifaa tiba TMDA Kanda ya kusini imeteketeza dawa na vifaa tiba vilivyoisha muda wa matumizi yake vyenyethamani ya Zaidi ya milioni mia tatu katika Hospitali ya misheni ya Nyangao Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi.



Akizungumza wakati wa zoezi hilo lililofanyika jana hospitalini hapo  mkaguzi wa dawa na vifaa tiba ofisi ya TMDA kanda ya kusini Elias Magambo amesema dawa hizo zilizoteketezwa ni mali ya Hospitali ya nyangao ambazo zimeisha muda wa matumizi yake.


Magambo alisem Miongoni mwa kazi za mamlaka hiyo ya TMDA ni kusimamia kazi ya zoezi la utekezaji na uhalibuji wa bidhaa za Dawa na vifaa tiba na vitendajishi ambavyo vimeisha muda wake wa matumizi  kama walivyofanya katika hospital hiyo .


" ki msingi dawa hizi zimeisha muda wake wa matumizi au hazifai tena kwa matumizi  kwa hivyo sisi kama mamlaka  kwa sababu tunasimamia usalama na ubora lakini lengo kuu la mamlaka hii ni kusimamia Afya ya jamii ya watanzania  , hivyo tunaamini kwamba bidhaa hizi  kwa kuwa zimeisha muda wake wa matumizi hazifai tena  kwa ajili ya kutumika ya binadamu"


Kwa upande wake Mfamasia kiongozi wa hospitali ya Nyangao Andrea Alfani amesema miongoni mwa dawa na vifaa tiba vilivyoteketezwa ni pamoja na dawa za maabara, dawa za vidonge na maji pamoja na vifaa tiba. 



Kwa upande wake Mfamasia kiongozi wa hospitali ya Nyangao Andrea alfani amesema miongoni mwa dawa na vifaa tiba vilivyoteketezwa ni pamoja na dawa za maabala, dawa za vidonge na maji pamoja na vifaa tiba. 


"Zipo sababu mbalimbali zilizofanya vifaa hivyo kupita muda wake moja ni dawa nyingi zilizoteketezwa ni zilizotokana na msaada  kutoka ujerumani na nchi zingine wanazotoka wahisani wetu na hii ni kutokana na kufika hapa hospitalini kwetu muda mchache kabla ya muda wa matumizi yake kupita na hivyo zikashindwa kutumika zote" 



"Zingine ni za programu mbali mbali za Serikali ambazo zinalipiwa na serikali kwa mfano Dawa za kutobu malaria na ARVS ambazo na zenyewe zinakuwa na sababu mbali mbali ambazo zinafikia kupita matumizi yake moja ni kubadilika kwa mtaala wa matumizi nyingine ni ile ya push system ambapo zamani MSD walikuwa wanaleta dawa pasipo sisi kuwapelekea mahitaji.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI