Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesema imeanza kufanya uchunguzi wake huru lengo likiwa ni kubaini ukweli kuhusu taarifa ya ajali ya gari iliyomuhusu Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Afya) Dkt Festo Ndugange iliyotokea katika Jiji la Dodoma na kuthibitishwa na Jeshi la Polisi.
Hayo yamebainishwa leo jijini hapa na Jaji Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mathew Mwaimu wakati alipokuwa Akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema Tume imeona taarifa kupitia vyomba vya mbalimbali vya habari hususan mitandao ya kijamii kuhusu kifo Cha mwanafunzi wa chuo kikuu Cha Dodoma (UDOM)Nusura Hassan Abdallah aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kawanza katika chuo hicho.
Ameeleza kumekukuwepo na taarifa ambazo kwa tafsiri yake zinaonekana kukinzana na zimekuwa zikikaririwa kutoka katika jeshi la polisi,chuo kikuu Cha Dodoma, Hospitali ya Faraja iliyopo Himo mkoani Kilimanjaro na taarifa za wananchi kupitia mitandao ya kijamii.
Amesema Kwa mujibu wa taarifa,inadaiwa kuwa Nusura alifariki katika hospitali ya Faraja,Himo mkoani Kilimanjaro.
"Kwa Hali yoyote Ile taarifa za kifo Cha mwanafunzi huyo ni za kusikitisha kwa kuwa kifo hicho,iwe kwa sababu yoyote Ile kimekatisha ndoto ya maisha yake na haki yake ya kupata elimu ya juu," Amesema Mwenyekiti huyo .
"Tume ya Haki za Binadamu inatambua kuhusu uwepo kwa vyomba vya habari vinavyoshugulikia masuala ya haki janai kuhusu jeshi la polisi na Ofisi yataifa ya mashtaka ambapo katika Mazingira ya kawaida vyomba hivyo vinahusika kulishugulikia Suala hili," Amesema
Amesema kwa kutambua Hilo tume inavipa heshma vyombo hivyo katika utekekezaji wa majukumu yake na kazi kubwa ambayo vinafanya.
Hata hivyo Amesema kunapotokea mashaka kutoka kwa wananchi kuhusu Jambo lolote linaloashiria uvunjwajiwa haki za Binadamu au mashaka ya haki kutokutendeka tume inayo mamlaka ya kufanya uchunguzijuu ya Jambo hilo kwa mujibu wa katiba na sheria ya tume kwakuwa inajukumu la kutetetea na kukinda haki za Binadamu nchini.
"Kwa Mujibu wa Kifungua Cha 1 Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Sura ya 391 Tume inayo mamlaka ya kuanzisha uchunguzi wake wenyewe juu ya malalamiko yanayoashiria uvunjifu wa haki za Binadamu na ukiukwaji wa msingi ya utawala Bora pasipo kusubiri kuletewa malalamiko.
0 Comments