Header Ads Widget

MWENYEKITI KIVUYO AKUSUDIA KIKUNDI CHA KIJAMII KUPITIA WHASSAP CHA MUSOMA YETU KUNUFAIKA KIUCHUMI

 


Na Shomari Binda-Musoma 

KIKUNDI cha kijamii kupitia Whassap cha Musoma Yetu kimeweka malengo ya baadae kuwa taasisi ndogo ya kifedha itakayoinua wanachama wake kiuchumi.

Hayo yamesemwa jana juni 14,2025 na Mwenyekiti wa kikundi hicho Cleopa Kivuyo wakati wa uzinduzi rasmi uliofanyika kwenye ukumbi wa Le Grand Beach.

Amesema lengo la kuanzishwa kwa kikundi hicho ni kusaidiana kwenye shida na raha na sasa baada ya kwenda vizuri wanakuja na mawazo makubwa ya kuwa taasisi ya kifedha.

Kivuyo amesema hawawezi kubaki kwenye kuchangiana kwenye misiba na sherehe lazima kila mwana kikundi amiliki uchumi hata kwa kukopeshana kwa riba nafuu.


Amesema jambo hilo linawezekana na kuwaomba wana kikundi kuwapa viongozi ushirikiano pale michakato hiyo itakapoanza.


Mwenyekiti huyo amewashukuru wana kikundi kwa kushiriki vyema matukio yakiwemo ya misìba na sherehe tangu wameanzisha na kuamini hata mambo makubwa wanayokusudia kuyafanya yatafanikiwa.


" Niwashukuru sana wana Musoma Yetu kwa kuifikia siku hii ya leo na kufanya uzinduzi rasmi wa umoja wetu ambao haubagui masikini wala tajiri.


" Tumshukuru sana mweka hazina wetu Andrew Laiser ( Kimotco) hatupo nae leo kutokana na majukumu ya kazi lakini amesimamia vyema michango hadi kufikia siku nzuri ya leo",amesema.


Katibu wa kikundi hicho Lameck Magoro amewaomba wana kikundi kuendelea kushirikiana na kuwa tayari kushiriki michango ya aina mbalimbali pale inapojitokeza

Magoro amewashukuru wana kikundi hao waliopo mji wa Musoma na waliotoka Mwanza na Tarime kwa kushiriki kwa pamoja tukio hilo.

Baadhi ya wana kikundi wametoa maoni yao kuboresha uendeshaji wa kikundi hicho na kuushukuru uongozi kwa kusimamia vyema tangu kuanzishwa kwake.

David Obambo mmoja wa wa wana kikundi hao amesema wanafurahia uwepo wa kikundi hicho na kudai watawapa ushirikiano viongozi wao na kuomba upendo kwa wana kikundi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI