Header Ads Widget

RC SENDIGA AWASHAURI WAKUU WA WILAYA KUTUMIA VYOMBO VYA HABARI KWA UFASAHA



NA: FRANCO NKYANDWALE: MATUKIO DAIMA APP  RUKWA. 

Mkuu wa Mkoa Rukwa Queen Sendiga amewataka Wakuu wa Wilaya zote za Mkoani Rukwa kutenga muda wa kuwasiliana na kufanya kazi na wanahabari kwa ufasaha ili kuibua changamoto zenye kuchochea maendelea Mkoani Rukwa humo na kuwafanya wananchi kuwa katika hali njema kiuchumi.


 Ushauri huo umetolewa leo wakati wa Maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani ambapo kimkoa yamefanyika leo tarehe 13, Mei mwaka huu.


Aidha amesema kwamba, wanahabari watumie kalamu zao vizuri kupiga vita ukatili wa kijinsia, kwani kwa sasa hali imekuwa tete kiasi kwamba wadau wote wakiwepo wanahabari wanatakiwa kushirikiana katika jambo ambalo litaufanya mkoa Mkoa utakuwa salama.



Kwa upande wake Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi kutoka Dawati la Jinsia Wilaya Sumbawanga Tabia Bakari amewashukuru wanahabari wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano mzuri katika suala la kupinga ukatili wa kijinsia, kwani Jeshi la Polisi peke yao hawataweza.


 Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Rukwa katika Maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani imewaalika wadau mbalimbali ili kujadili changamoto ambazo zinaukabili Mkoa wa Rukwa katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Mkuu mkoani humo.


Kauli mbiu ya 2023 ikiwa ni "KUUNDA MUSTAKABALI WA HAKI,UHURU WA KUJIELEZA KAMA KICHOCHEO CHA HAKI NYINGINE ZOTE ZA BINADAM".

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI