Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa Mrakibu wa Polisi SP Mossi Ndozero amewataka madereva na waongoza njia (navigators) wa mbio za magari kuhakikisha wanakua makini wawapo katika mashindano pamoja na washiriki wa mashindano hayo kuhakikisha wanaweka usalama kwanza ikiwa pamoja na kufuata sheria za usalama barabarani.
Akizungumza Mei 13, 2023 baada ya kuzinduliwa rasmi kwa mashindano hayo katika hoteli ya Mout Rayal iliyopo Gangilonga Mkoani Iringa ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika kesho Mei 14, 2023 katika Shamba la Miti Sao Hill lililopo Wilayani Mufindi linalomikiliwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Aidha, SP Ndozero amesema ulinzi utaimarishwa muda wote hadi mashindano hayo yatakapokamilika.
0 Comments