Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM - MATUKIO DAIMA
IKIWA yamebaki Masaa Machache kwa Klabu ya Yanga kushuka Dimbani Benjamini Makapa kucheza Mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Fainali dhidi ya USM Alger ya Algeria, Mashabiki wa Yanga wameibuka kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa hamasa yake katika michezo.
Mashabiki wa Yanga Wamejitokeza leo katika Viwanja vya Zakhem Mbagala Jijini Dar Es Salama wakati wa Shamrashamra kuelekea Mchezo wa Fainali unaotarajiwa kuchezwa Mei 28 mwaka Huu, Mashabiki hao walibeba Mabango yaliyokuwa na Ujembe mbalimbali wa kumshukuru Rais Dkt Samia.
Rais Samia Suluhu Hassan chini ya Serikali ya Awamu ya Sita anayoiongoza amefanikisha hamasa kwa timu kuingia Uwanjani ikiwa na sapoti ya taifa,Ikumbukwe kuwa, Rais Samia alianza hamasa kwa kutoa fedha kiasi cha Shilingi Milioni Tano kwa kila Goli lililofungwa na Klabu ya Simba na Yanga wakiwa katika Makundi ya Mashindano ya Afrika na Shilingi Milion 10 kuanzia nusu fainali kwa kila bado.
Aidha Rais Dkt Samia ameweka ahadi kutoa Shilingi Milion 20 kwa kila bao la ushindi litakalofungwa katika Mchezo wa fainali pamoja na kununua tiketi 500 kwa Mashabiki wa Timu hiyo.
Sambamba na hayo Rais Dkt Samia ameongeza Shangwe kwa Mabingwa wa Kihistoria Klabu ya Yanga kwa kutoa ndege kwa Mashabiki wa Timu hiyo kwenda Algeria katika Mchezo wa Mkondo wa Pili wa Fainali ambao unatarajiwa kuchezwa June 03 mwaka huu.
Mapema akizungumza na Waandishi wa Habari Rais wa Klabu ya Yanga Eng Hersi Said alisema kuwa, Yanga imehemewa kwa hatua ya Rais Samia kwa kuongeza hamasa yake pamoja na kutoa ndege ambapo mambo hayo mawili yanawafanya sasa kuogeza umakini katika kuhakikisha wanaleta kombe Nyumbani.
"Tunachokisema kama Yanga Tutarudi Nyumbani na hatutamuangusha Rais Wetu katika Mchezo yote Miwili ya Fainali na kuhakikisha tunaleta kombe nyumbani Tanzania,"alisema Hersi Said.
Hatua inayokuja ni fursa si kwa Yanga kama timu bali Tanzania kama Taifa na Nchi kwa kuwa Wenyeji wa Fainali za Afrika. Fursa hii imekuja kwa gharama kubwa ya Serikali chini ya Uongozi wa Dkt Samia, Uwekekezaji Mkubwa wa Klabu ya Yanga, Uongozi Mahiri na Uimara wa Benchi la Ufundi a Wachezaji wa Klabu hiyo.
0 Comments