Header Ads Widget

CHONGOLO ASEMA CCM TAYARI IMEMPA RIDHAA RAIS DR SAMIA KUENDELEA NA MCHAKATO WA KATIBA WENGINE WASIDANDIE

 


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema suala la Mchakato wa katiba mpya ni ajenda yao na kuwa Mchakato huo ulianza mapema na hao wanaosikika Sasa wakidai katiba mpya ndio waliosusia bunge la katiba na kutoka nje ya bunge ila shauku ya CCM kupata katiba Bora na sio Bora katiba .

Kauli hiyo Imetolewa Leo Ijumaa Mei 26 ,2023 wilayani Mufindi mkoani Iringa na katibu mkuu wa CCM Taifa Daniel Chongolo wakati akiwasalimia wanaccm waliojitokeza kwenye Mapokezi yake .

Chongolo alisema kuwa  CCM kimeshampa ridhaa na dhamana mwenyekiti wao, Rais Dk Samia Suluhu Hassan kuanzisha mchakato huo.

Alisema kuwa wamesikia huko watu wanazungumza wanataka katiba mpya ila ukweli wanadandia ajenda ya CCM 

Alisema wakati CCM inajadili namna kuendeleza mchakato huo ulisimama kwa miaka tisa bado kuna wachache wanaotaka jambo hilo lionekane kama lao wakijiita sisi ni sisi.

Katika mchakato huo, Chongolo alisema CCM inayo dhamira ya dhati na ya kweli itakayohakikisha Tanzania inapata Katiba mpya na bora.

Amewataka watanzania kuachana na wanasiasa wanaotoa ahadi hewa akisema katika mchakato wowote wa maendeleo hakuna miujiza kwa watu wasiofanya kazi.

Alisema chama hicho sio cha kurukaruka hewani kama nyani au ngedere kwani kina uzoefu wa uongozi na kinatambua mahitaji ya wananchi wake.

“Mimi na timu yangu tumekuja Iringa kukagua utekelezaji wa Ilani yetu kwasababu tuliahidi na tunajua watanzania wanataka maji, umeme, elimu, huduma za afya, barabara na huduma zote za kijamii,” aliongeza Chongolo.

Katika ziara yake mjini Mafinga kesho Chongolo atazindua mradi wa vibanda vya CCM, nyumba ya Katibu wa CCM, kushiriki ujenzi wa maji miji 28, kituo cha Afya Ifingo na kugawa vyandarua na baadaye kufanya mkutano wa hadhara..

Katika ziara hiyo Chongolo ame



ongozana na sekretarieti ya CCM Taifa akiwemo Katibu wa itikadi na uenezi Taifa Sophia Mjema na wengine huku akipokelewa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Daud Yasin,Wajumbe wa NEC Leonard Mahenda na Salim Abri Asas na Viongozi wengine wa chama na Serikali mkoa wa Iringa .






















Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI