Header Ads Widget

OSHA WAJIPANGA KUTOA ELIMU KATIKA VIWANDA KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA NA USALAMA




NA CHAUSIKU SAID

MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.


Wakala wa usalama na afya mahali pa kazi Mkoa wa Mwanza(OSHA) wamejipanga kutoa elimu katika viwanda vya Sayona steel, Nyakato steel pamoja na mwatex.


Akizungumza na matukio daima Meneja wa OSHA Kanda ya ziwa Mjawa Mohamed Amesema kuwa lengo la kutoa elimu hiyo Kwa wafanyakazi wa viwanda hivyo ni kuwasaidia wafanyakazi hao  kufanya kazi Kwa ufanisi na Kwa kuzingatia Afya zao.


"Tumeona pia twende kwenye kiwanda pia kinachotengeneza nguo mashine zile Zina kelele sana na vumbi la pamba Kwa hiyo haya maeneo tumeona kwamba ndio yanaviatarishi inabidi tuwape elimu" Alisema Mohamed.


Mohamed ameeleza kuwa elimu watakayowapa wafanyakazi hao itawapa uwelewa na kuwa na uwezo wa kufahamu ambacho wanapaswa kufanya Kwa kuzingatia uweledi pamoja na kizifahamu haki zao na wajibu wao unaohusu Afya na Usalama mahali pa kazi.


" Lengo la kutoa elimu ni kuhakikisha wanapata elimu, unajua mtu akishapata elimu na kizifahami haki zake na wajibu wake ni upi na majukumu yake ni yapi yeye kama mfanyakazi atafanya kazi vizuri" Alisema Mohamed.


Mohamed ameeleza kuwa sheria inampataka mfanyakazi kupata elimu ambayo itamsaidi kufanya kazi na kifungu Cha 95 kinamtaka mfanyakazi kufahamu wajibu wa  kujilinda na kuwalinda wenzake katika eneo la kazi na elimu hiyo inaweza kumsadia kutoa taarifa pindi anapoona kiatarishi mahala pa kazi.


Hata hivyo maadhimisho ya siku ya Afya na Usalama mahali pa kazi yatafanyika April 28 katika viwanja vya tumbaku Mjini Morogoro.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI