NA CHAUSIKU SAID
MATUKIO DAIMAAPP MWANZA
Wakazi wa Busenga kata ya Buswelu Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza wameiomba serikali kuwatengenezea miundombinu rafiki ya Barabara itakayo wasaidia kupita Kwa urahisi hususani katika kipindi Cha mvua na kuepukana vifo vya watoto visivyotarajiwa.
Hayo yamejiri baada ya mvua kunyesha na kusababisha barabara ya mtaa Angelina Mabula kutopitika na kupelekea kuzama Kwa magari na kusababisha watoto kutoenda shule na shughuli nyingine kutofanyika.
Mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi tawi la Busenga Faisal Modest ameeleza kuwa mtaa huo kutokana na miundombinu kuwa mibovu mvua ikinyesha wanapata mafuriko yanayowaasili wakazi wa eneo hilo.
"Tunaishi Busenga mtaa ambao Ninaweza kusema Kwa namna moja au nyingine tumetengwa " Alisema Modest.
Ameiomba serikali kutengeneza barabara hiyo ili mvua zinaponyesha zisiendelee kusababisha mafaha Kwa watoto na wakazi wanayoishi katika maeneo hayo hali inayopelekea wananwake na watoto kupata changamoto ya kushindwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
"Juzi tu mvua kama hii ikinyesha na kusababisha kifo Cha Mtoto mdogo wa mwaka mmoja na miezi nane, tusipoweza kujenga barabara hizi na kuweza kuthibiti haya maji wakazi wa Busenga tutaendelea kupata athari" Alisema
Kwa upande wake Balozi wa mtaa huo Michael Duke ameeleza kuwa kutokana na miundombinu mibovu ya barabara hiyo hupelekea watoto kutoenda shule.
" Busenga imekuwa kama dampo maji yote yanayotoka viwandani yanaishia huku Kwa sababu miundombinu mibovu hivyo hupelekea wananchi kupata fangasi na maji kuingia ndani" Alisema Duke.
Sharifa Idrissa mkazi wa eneo hilo na Ayubu Mohamed wanafunzi wa darasa la nne wameeleza kuwa kutokana na mvua zinazonyesha wanapata adha ya maji kuingia ndani na nyumba kubomoka uwezo wa kuyazuia hawana pamoja na wanafunzi kupata changamoto ya kwenda shule.
"Tunaomba tutengenezewe hili barabara na tuwekewe madaraja pale panapositahili kuwekwa"Wakisema.
Hata hivyo wananchi hao wote Kwa pamoja wamepaza sauti zao na kumuomba Mbunge wa eneo hilo Angelina Mabula kuhakikisha anawatengenezea miundombinu ya barabara hiyo ili iweze kuwa msaada Kwao.
0 Comments