Header Ads Widget

MBUNGE ZUENA BUSHIRI AIPIGIA DEBE BARABARA YA KIA-SANYA JUU.

 


NA WILLIUM PAUL.


MBUNGE wa Viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri ameikumbusha Serikali ahadi ya Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ya ujenzi wa barabara ya Kia kwenda Sanya juu.

Barabara hiyo ambayo ikijengwa itasaidia kufungua utalii wa Mlima Kilimanjaro kwa wageni kupitia njia hiyo kwenda mlima Kilimanjaro.

Mbunge huyo akiuliza swali leo Bungeni kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Atupele Mwakibete ni lini Serikali itajenga barabara ya Kia kwenda Sanya juu kwa kiwango cha lami ambapo ni ahadi ya Rais Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.


Akijibu swali hilo Naibu Waziri alimwomba Mbunge Zuena kuvuta subira mpaka watakaposoma bajeti ya Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano ambapo watatoa mapendekezo nini kifanyike katika barabara hiyo.

Kujengwa kwa barabara hiyo kutasaidia kufungua maendeleo kwa wananchi wa wilaya za Hai na Siha mkoani Kilimanjaro pamoja na Taifa kutokana na kutumiwa na wageni kupanda mlima Kilimanjaro.

Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI