Header Ads Widget

NUSU YA WAKAZI DUNIANI WANATARAJIWA KUWA NA UZITO WA JUU ZAIDI WA MWILI MWAKA 2035


Zaidi ya nusu ya watu duniani watakuwa na uzito mkubwa wa mwili kufikia mwaka 2035 iwapo hatua kudhibiti hilo hazitachukuliwa, limetahadharisha shirikisho la kupambana na unene wa mwili wa kupindukia duniani, (World Obesity Federation ).

Ripoti ya shirikisho hilo imesema, Watu zaidi ya bilioni nne wataathiriwa, huku viwango vikitarajiwa kuongezeka kwa kasi zaidi miongoni mwa watoto.


Nchi zenye kipato cha chini na cha kati barani Afrika na Asia zinatarajiwa kushuhudia ongezeko kubwa zaidi la watu wenye uzito wa mwili wa kupindukia.


Ripoti hiyo, inabashiri kuwa garama ya unene wa mwili wa kupindukia itapanda na kufikiza zaidi ya dola trilioni 4 za Kimarekani (£3.3tn) kila mwaka ifikapo 2035.


Pia, imeelezea hasa kuongezeka kwa viwango vya uzito wa mwili wa kupindukia miongoni mwa watoto na vijana wadogo wenye umri wa kubalehe, huku viwango vyao vikitarajiwa kuongezeka mara dufu ikilinganishwa na viwango vya mwaka 2020 miongoni mwa wavulana na wasichana.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI