Header Ads Widget

KAMATI YA PAC YAPONGEZA UJENZI WA BARABARA YA LAMI YA NJOMBE MAKETE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali PAC imekiri kuridhishwa na ujenzi wa barabara ya Njombe Makete Km 107.4 kwa kiwango Cha lami huku ikiwataka watumiaji kuitunza  vizuri.


Baada ya Kamati hiyo kuzulu mkoani Njombe kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo barabara hiyo makamu mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Japheth Hasunga mbunge wa Jimbo la Vwawa amesema baada ya kufanya ukaguzi huo pamoja na kupitia ripoti ya CAG wamejiridhisha na ujenzi huo ambao sasa umepunguza machungu ya kutumia gharama kubwa ya nauli kwa wananchi.


Mhe.Hasunga amewaagiza madereva kuzingatia alama za usalama barabarani pindi wanapoendesha vyombo vya Moto huku akiwataka wananchi kuitunza ili idumu kwa miaka mingi.



Awali Mtendaji mkuu wa barabara nchini Mhandisi Rogatus Mativila amesema barabara hiyo ya Njombe Makete ilijengwa kwa kugawanywa katika sehemu kuu mbili ambapo sehemu ya Kwanza ni Njombe Moronga Km.53.9 na sehemu ya pili ni Moronga Makete Km 53.9 na zilishakamilika na zinafanyakazi vizuri.


Mhandisi Mativila amesema barabara hiyo iliyojengwa na wakandarasi wawili tofauti imegharimu kiasi Cha shilingi bilioni 243 na kukamilika Agosti 31 mwaka 2022.



Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga ambaye Ni mbunge wa Jimbo la Makambako amesema fedha zilizoletwa na  serikali kwa ajili ya ujenzi wa barabara zimesaidia sana barabara kufunguka kwani kwa wakazi wa makete kwenda mbeya hawalazimiki kuzunguka tena Njombe.


Baadhi ya wananchi mkoani Njombe akiwemo Isabela Msemwa wamesema kujengwa kwa barabara hiyo kwa kiwango Cha lami kumewarahisishia safari ya Njombe Makete ukilinganisha na miaka michache iliyopita kabla ya kujengwa kwani hivi sasa hata nauli zimepungua na wanafurahia maisha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI