Header Ads Widget

WAZIRI MAJALIWA KUSOMESHA WATOTO WA HAYATI ABDULAZIZ AHMEID ALIEKUWA MWANDISHI WA HABARI WA CHANEL TEN LINDI.

 


Na HADIJA OMARY LINDI.



WAZIRI Mkuu Kassimu Majaliwa amehaidi kubeba jukumu la kuwahudumia watoto wawili wa aliekuwa  mwandishi wa Habari wa Kituo cha Chanel ten Mkoani Lindi ,marehemu Abdullazi Ahmadi,kwa kuwasomesha hadi watakapo hitimu masomo yao.


Waziri Majaliwa ameitoa ahadi hiyo Mkoani Lindi,alipokuwa anatoa salamu za pole kwa wafiwa, wakati wa mazishi ya mwandishi huyo,yaliyofanyika makaburi eneo la Mitandi  katika Manispaa hiyo.



Waziri mkuu amesema kufuatia mahusiano mazuri yaliyokuwepo kati yake na mwandishi wa Habari huyo wakati wa uhai wake,ameahidi kuendelea kuchukuwa jukumu la kuwasomesha watoto wawili wa marehemu Abdullaziz hadi watakapomaliza masomo yao ambao ni Ahmad Abdullaziz aliemaliza masomo yake ya kidato cha nne Shule ya Sekondari ya Nyangao iliyopo Halmashauri ya Mtama  Nurudini Abdullaziz  anaesoma katika shule ya wonder kids iliyopo Wilayani Ruangwa. 



Amesema wakati wa uhai wake,mwandishi huyo amewahi kushika nyazifa mbalimbali,zikiwemo za siasa,kwa nafasi  ya mjumbe wa kamati kuu ya Taifa Chama cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya Wilaya na kuwa mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Lindi (LRPC).




“Kufuatia mahusiano mazuri na marehemu Abdullaziz Ahmad napenda kuhaidi nitaendelea kuwasomesha watoto wale hadi watapomaliza masomo yao”Alisema waziri mkuu Majaliwa.


Kwa upande wake Baba mdogo wa marehemu Abdullaziz ,Mohamedi Abdullaziz, akizungumza kwa niaba ya familia, amemshukuru Waziri mkuu Kassimu Majaliwa,kwa ushirikiano aliouonyesha wakati kijana wao akiwa amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akipata matibabu kwa tatizo lililokuwa linamsumbua.



“Kwa niaba ya familia,nachukuwa nafasi hii kukushukuru waziri mkuu kwa kazi kubwa uliyoifanya,ikiwemo kushiriki gharama za matibabu za kijana wetu”Alisema Mohamedi Abdullaziz.



Aidha,Mohamedi Abdullaziz aliyewahi kuwa M’bunge wa Jimbo la Lindi mjini kwa kipindi cha miaka (15) na mkuu wa Mikoa ya Tanga na Iringa amempongeza Waziri mkuu kuendelea kubeba jukumu la kuwasomesha watoto wa marehemu hadi pale watakapohitimu masomo yao.




Marehemu  Abdullaziz ameacha mke mmoja na watoto wanne ,Ahmad Abdullazizi, Nurudini Abdullaziz,  Shekha Abdullaziz na Bakari Abdullaziz. 


Marehemu Abdullaziz Ahmadi alikuwa anasumbuliwa na tatizo la Kongosho na kulazwa  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu  hadi Machi 13 mwaka huu,alipofariki dunia na kuzikwa mjini Lindi Machi 14/2023 saa 11:30 za Alasiri, mwenyezi mungu ailaze roho yake mahali pema.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI