Header Ads Widget

ASKARI POLISI WAWILI WAFARIKI KWENYE AJALI MWINGINE AJERUHIWA.

 


ASKARI wawili wa Kituo cha Kiwilaya Kipolisi  Chalinze na karani wa Mahakama ya Mwanzo Lugoba wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa katika ajali ya gari.


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ACP Pius Lutumo amesema kuwa watu hao walifariki baada ya gari dogo walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.


Lutumo amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo Machi 5 mwaka huu majira ya saa 11:45 alfajiri huko maeneo ya Mavi ya Ng'ombe Kijiji cha Mboga Kata ya Msoga Tarafa ya Chalinze katika Barabara ya Chalinze/Segera.


Amesema kuwa ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili T 323 BAL aina ya Toyota Cresta likiendeshwa na mkaguzi msaidizi wa Polisi Ndwanga Dastani (28) askari wa kituo cha Polisi Chalinze akitokea Chalinze kuelekea Lugoba liliacha njia kutoka upande wa kushoto wa barabara na kwenda upande wa kulia na kugonga kalavati kisha kupinduka na kusababisha vifo vya watu watatu na mmoja kujeruhiwa .


Amewataja askari waliokufa kuwa ni Mkaguzi msaidizi wa Polisi Ndwanga Dastani (28) aliyekuwa dereva wa gari hilo, Konstebo  Emmiliana Charles (26) wote askari wa kituo cha Polisi Chalinze na Karimu Simba (27) ambaye ni karani wa Mahakama ya Wilaya Lugoba ambapo majeruhi ni askari wa Kituo cha Polisi Chalinze Konstebo Mwanaidi Shabani (25) ameumia maeneo mbalimbali ya mwili wake na amepelekwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.


Amesema kuwa uchunguzi wa awali umeweza kubaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na dereva kushindwa kulimudu gari na kupinduka.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI