Amon Mtega ,Mbinga.
MENEJA wa Wakala wa barabara za Mijini na Vijijini Tanzania (TARURA) Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Oscar Mussa amewaondoa hofu madiwani wa Halmashauri ya Mbinga Mji kuwa katika makisio ya rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2023 na 2024 itazingatia maeneo mbalimbali ya Miundombinu ikiwemo ya madaraja na barabara za maeneo korofi.
Mussa amewaondoa hofu hiyo wakati akiwasilisha makisio ya rasimu ya bajeti hiyo ambayo ya Tzs 2,441,127,000.00 zikipishwa zita tarajia kutengeneza Miundombinu mbalimbali ya barabara katika maeneo mengi ya Halmashauri hiyo.
Akiwasilisha makisio ya rasimu ya bajeti hiyo kwenye kikao cha Baraza la madiwani kilichohudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Aziza Mangosongo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Mbinga mjini Jonas Mbunda amesema kuwa licha ya bajeti hiyo kutengeneza Miundombinu mbalimbali ya barabara lakini itajengwa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa km,1.7 ambayo itakuwa imeongeza idadi ya mtandao wa barabara za lami kwenye Halmashauri ya Mbinga Mji.
Aidha Meneja huyo amepongeza Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022 na 2023 Rais huyo aliongeza fedha Tzs 1,500,000,000.00 ambazo zimetumika kuongeza mtandao wa barabara.
Hata hivyo amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Mbinga mjini Jonas Mbunda pamoja na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Kevin Mapunda , Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Grance Quintene pamoja na madiwani kwa ushirikiano wanaoufanya katika ofisi ya Tarura.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Kevin Mapunda akizungumza baada ya kuwasilishwa kwa rasimu ya bajeti hiyo amewapongeza Tarura kwa kazi wanazozifanya huku akiwataka waongeze bidii kuyashughulikia maeneo korofi ya barabara kwa wakati.
0 Comments