Header Ads Widget

MHE. OTHMAN AWATAKA WAGONJWA KUWA NA SUBRA.

 



Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Machi 05, 2023 amefika na kuwajulia hali wananchi mbali mbali katika vijiji vya Micheweni.

 

Katika ziara hiyo, Mhe. Othman amemjulia hali Bw. Ramadhan Saleh Faki wa Maziwang'ombe na Bw. Hamad Fundi Kombo wa Chamboni- Micheweni wote wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.


Akitoa salamu zake za pole kwa wananchi hao wanaosumbuliwa na maradhi mbali mbali, Mhe. Othman amewanasihi wazidishe subra kwani maradhi ni sehemu ya mitihani anayojaribiwa mja kutoka kwa Mola Mwenyezi, na kuahidi kuendeleza utamaduni wa kuwa pamoja nao kama ambavyo amerithi mwenendo huo kutoka kwa Viongozi waliomtangulia.



Kwa nyakati tofauti wajuliwa hao wametoa shukran zao za dhati, kwa kiongozi huyo, kufuatia kitendo hicho, ambapo miongoni mwao Mzee Ramadhan Saleh Faki amekaririwa akisema; "umefanya jambo jema kuendeleza mirathi ya mtangulizi wako Maalim Seif Sharif Hamad, maana hizi ni katika akhlaki (tabia) njema zenye kumpendeza Mwenyezi Mungu Muumba".





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI