NA AMINA SAIDI,TANGA
Halmashauri ya jiji la Tanga imewaelekeza wafanyabiashara wa jiji la Tanga wanaofanya biashara katika maeneo ya barabara zisizofungwa kwa matumizi hayo waache mara moja na kuhakikisha zinakuwa salama kwa matumizi ya vyombo vya moto.
Hayo aliyasema mstahiki Meya wa jiji la Tanga Abdarahman Shillow katika baraza la madiwani la Halmashauri ya jiji Tanga ambapo aliwaomba mkurugenzi wa jiji pamoja na uongozi wake wote kulisimia suala hilo.
Aidha alisema kuwa wafanyabiashara kufanya biashara nje ya maduka yao na kuweka barabarani ni kuhatarisha maisha ya watumiaji wa barabara hizo pamoja na watumiaji wa vyombo vya moto.
Aliwaomba watendaji wote wa halmashauri kwa kushirikiana na Mkurugenzi wajiji Bi.Sipora Liana kuweza kulisimamia hilo kwa yoyote atakaekiuka maelekezo hayo achukiliwe hatua za kisheria.
Sambamba na hayo katika baraza hilo mstahiki meya wa Jiji la Tanga pamoja na mkurugenzi walimpongeza Diwani wa kata ya Mnyanjani kayaga simba ambaye alichukukua nafasi aliyekuwa Diwani kutangulia mbele ya haki.
Mh.Simba alipita kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika mwishoni mwa mwezi wa kumi na mbili mwaka uliopita kupitia tiketi chama cha mapinduzi CCM mkoa Tanga.
Aidha katika baraza hilo pia mh.Kayaga Simba aliapishwa kwenye baraza hilo na kushiriki baraza la madiwani akiwa kama diwani wa kata ya mianjani kupitia Chama tawala CCM.
Akizungumza mara baada ya baraza hilo Diwani Simba alisema yupo tayari kushirikiana wananchi wa kata ya mianjani katika kuhakikisha kero zao zote zinapatiwa majibu kama ilivyo ilani ya chama chama mapinduzi.
0 Comments