Header Ads Widget

UINGIZAJI NGURUWE MBARALI WAPIGWA MARUFUKU

 



Na Matukio daima media , Mbarali


HALMASHAURI ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya imepiga marufuku usafirishaji wa wanyama aina  ya nguruwe kutoka eneo moja hadi lingine kutokana na kuibuka  mlipuko wa  ugonjwa wa homa  ya nguruwe kutoka Mji makambako mkoani Njombe na Mafinga Mji katika mkoa wa Iringa Pamoja na  Jiji la Mbeya .


Akizungumza leo wakati wa akitoa taarifa za ugonjwa huo kwenye kikao cha baraza la madiwani cha kawaida  ,Mkuu wa Idara ya kilimo na mifugo  na uvuvi ,Dkt.Anania  Sangwa amesema kuwa katika maeneo ambayo yanazungukwa na wilaya ya mbarali kumetokea mlipuko wa ugonjwa wa homa ya Nguruwe  .



‘’Tumepata taarifa kuwa majirani zetu Mji Makambako , Mafinga, pamoja na Jiji la Mbeya kuna mlipuko wa ugonjwa wa homa ya Nguruwe na ukiangalia kwa Jiografia tuliyopo ni rahisi  sana kupata ugonjwa huu kwa namna unavyosambaa kwa kasi  wito wangu kwenu tusaidiane kupeleka taarifa hii kwenye maeneo yetu kwasasa haturuhusu tena usafirishaji wa Nguruwe  kutoka eneo moja hadi linguine , wanyama wote watakaguliwa wakiwa hai kwanza na  baada ya kuchinja tena watakaguliwa  kwa umakini mkubwa ,tunashauri wafugaji wetu wasipeleke mifugo kupandisha  kwenye sehemu zingine ni vema kujitegemea ‘’amesema Dkt. Sangwa.


Akielezea zaidi Dkt. Sangwa amesema pia waepuke kubeba makombo kupeleka nyumbani mara baada ya kula nyama hiyo  kwa lengo la kulisha Nguruwe kwani unaweza ukawa umebeba virusi vya homa ya  nguruwe na kusambaza zaidi   hivyo waepuke hilo , pia amewataka wamiliki wa  wa Nguruwe wahakikishe wanafanya usafi  kwenye mabanda  kwa kutumia dawa ili wote wapate elimu namna ya kujikinga na ugonjwa huo.



Aidha amesema kuwa kupitia kamati ya usalama wilaya  tayari imeanza kulifanyia kazi  kwa kuhakikisha kuwa vituo vyote vya mipakani kuwa kila Nguruwe anayepitishwa  mipakani , barabarani wanafanyiwa  ukaguzi na kama wafugaji wanasafirisha nguruwe wahakikishe wanakuwa na vibali kutoka kanda kwa ofisa mfawidhi  mkoa wa Iringa  ambao wanachukua sampuli za nguruwe.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbarali Twalib Lubandamo amesema kuwa mlipuko wa ugonjwa huu si mzuri  hivyo ni vema  wananchi kuchukua tahadhari .

‘’tusiache nguruwe hawa wakisambaa ovyo kuwe na sehem u ya kufugia ili kuepuka kusambaa kwa ugonjwa huu ambao tayari upo kwa majirani zetu mji makambako, Mafinga na Jiji la Mbeya’’amesema Mwenyekiti huyo.




Katibu Tawala wilaya ya Mbarali  amesema  ,Michael Semindu amesema kuwa  hatua zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya ugonjwa huo katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo  pamoja na kusimamia uingizaji kiholela wa nguruwe ikiwa ni pamoja na kusimamia  kwenye maeneo ya mipaka.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI