Header Ads Widget

MBUNGE ZUENA ATAKA WANAWAKE WAJITOSE KUWANIA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI.

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

WANAWAKE Nchini wametakiwa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa mwakani pamoja na uchaguzi Mkuu 2025.

Kauli hiyo ilitolewa na Mbunge wa viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri alipofanya mkutano wa hadhara kata ya Njoro wilayani Moshi ikiwa na lengo la kusikiliza kero na wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.



Zuena alisema kuwa, uchaguzi ndani ya chama umekwisha sasa uchaguzi unaoelekea ni Serikali za mitaa mwakani kwa ajili ya kuunda Serikali.


Alisema kuwa, uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 ni Dira ya chama kuelekea uchaguzi Mkuu 2025 na kuwataka wananchi na wanachama wa CCM kuhakikisha chama kinashinda kwa kishindo Serikali za mitaa.



"Wakinamama tunawajibu wa kumuunga mkono mwanamke mwenzetu Dkt Samia Suluhu Hasani kwa kujitosa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye chaguzi zinazokuja mbele yetu wanawake tunaweza" alisema Mbunge Zuena.

Aidha Mbunge huyo alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi katika kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto pamoja na wanawake.


Alisema kuwa, kumekuwepo na mfumuko wa vitendo vya ukatili hasa kwa watoto jambo ambalo halikubali katika jamii na kuwataka kuungana kuwafichua wale wote wanaofanya vitendo hivo.

Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI