NA CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Chama Cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza kinatarajia kufanya maadhimisho ya miaka 46 Kwa kuwatembelea watoto yatima na kutoa misaada pamoja na upandaji miti.
Haya yamebainishwa na Katibu CCM Mkoa Omary Mtuwa na kueleza kuwa Maadhimisho Hayo yanayotarajiwa kufanyika Februari 4 mwaka huu katika viwanja vya furahisha Wilaya ya Ilemela wataanza Kwa kuwakumbuka watoto hao.
Omary ameeleza kuwa Maadhimisho Hayo yataambatana na utoaji wa historia ya chama hicho tangu kilipoanza hadi sasa kilipofikia pamoja na ugawaji wa kadi Kwa wanachama wapya watakojiunga na chama hicho.
"Mzee wetu mmoja maarufu kutoka chama chetu ambaye pia amewahi kuwa katibu kutoka Mkoa wetu huu atatoa historia ya chama ili vijana kuweza kufahamu kiundani chama hicho" Alisema Omary.
Aidha ameeleza kuwa wanachama na wananchi Kwa ujumla wategemee kuona mabadiliko makubwa yatakayofanywa na chama Cha mapinduzi tangu kuasisiwa kwake.
"Ccm imefanya vitu vingi sana katika Nchi hii Mimi leo nina miaka 42 na Ccm Ina miaka 46 nimeishi Kwa ajili ya Ccm, nimesoma, nimetembea kwenye Barabara zilizojengwa Kwa ajili ya Ccm" Alisema Omary.
Kwa upande mwingine amewataka wananchi kujitokeza Kwa wingi siku hiyo ili kuweza kusikiliza sera ambazo zimeandaliwa Kwa ustadi pamoja na hotuba zikazojibu maswali huku Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo akitarajiwa kuwa Askofu Joseph Gwajima ambaye pia ni (MNEC)
0 Comments