Header Ads Widget

WADAU WA AFYA MOJA KUTOKA (EAC) WAKUTANA JIJINI ARUSHA KUJADILI MSTAKABALI WA MAGONJWA WA MLIPUKO

 




Teddy Kilanga ARUSHA


Wadau wa afya moja kutoka nchi za jumuiya ya Afrika ya Mashariki(EAC) wakutana jijini Arusha kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali na kujengeana uwezo namna ya  kukabiliana magonjwa ya mlipuko pindi yanapotokea katika maeneo ya nchi zao kwa lengo la kuhimarisha afya za viumbe hai ikiwemo binadamu na wanyama.


Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na serikali ya ujerumani(GIZ) Mtaalamu wa mifugo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Baltazary Leba amesema dhana ya afya moja inawasaidia kuhakikisha sekta mbalimbali zinaunganisha nguvu  katika kutatua changamoto ya afya kwa jamii.


"Na ili dhana hii iweze kutekelezwa katika nchi za EAC lazima serikali za nchi husika zishiriki katika kuchangia hupatikanaji wa rasilimali mbalimbali zitakazowasaidia wadau wa afya moja kukabiliana na magonjwa ya mlipuko pindi yatakapotokea katika nchi husika,"amesema Mtaalamu huyo.


Aidha amesema kuwa nchi ya Tanzania imefanikiwa kuhimarisha afya moja kwa jamii kutokana na serikali yake kuwa mstari wa mbele katika kusaidia upatikanaji wa rasilimali mbalimbali ikiwemo vifaa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.


Dkt.David Balkoa kutoka sekretarieti ya jumuiya ya Afrika ya Mashariki amesema nchi za EAC zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinaathiri sekta ya afya na mazingira kupitia wanyama ikiwa utafiti umeonyesha asilimia 65 ya magonjwa ambayo yanaathiri afya ya binadamu yanatoka kwa wanyama.



Dkt.Balkoa amesema mkakati wa afya moja kupitia sekta mbalimbali utasaidia kuhamasisha wataalamu kufanya kazi pamoja  kwa lengo la kuboresha afya ya jamii na mazingira kwa ujumla.


"Lengo kuu ya afya moja ni kuhimarisha afya kwa jamii sambamba na wanyama wafugwao kuepukana na magonjwa ya mlipuko yanayotokea katika mazingira ili yasiweze kuathiri uchumi wa nchi na wa mtu mmoja mmoja,"amesema

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI