Na Esther Machangu Matukio Daima Kilimanjaro
Mabadiliko ya teknolojia, elimu ya Biashara pamoja na uhamasishaji umechangia kwa kiasi kikubwa wanawake wengi kujikita katika kufanya Biashara, ndani na nje ya nchi.
Pamoja na mabadiliko yaho ya kiteknolijia Maswala ya ukatili wakijinsia yameanishwa kuwa ni chanzo Cha wanawake kujikita katika shughuli za ushalishaji Ili kuepuka utegemezi katika familia na kuondoka Changamoto za ukosefu wa kipato.
Mwajuma hamza, ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha wanawake wafanyabiashara Tanzania (Twcc) ameyasema hayo January 20,2023, katika kongamano la Wanawake wafanya Biashara, Mkoani Kilimanjaro likiwa na lengo la kutoa elimu na kubadilishana uzoefu katika Biashara.
Mwajuma amesema wanawake wafanya Biashara kwa sasa wanatakiwa kuzalisha bidhaa zinazokidhi viwango Ili ziweze kuwa na ushindani wa kitaifa na kimataifa kwani kwa sasa nchi ya Tanzania imeingia katika soko Huru la Afrika, hivyo ni lazima bidhaa zitakazo Toka nchi hapa ziwe zimezingatia viwango na ubora.
Mwenyekiti wa Chama Cha wanawake wafanya Biashara Mkoa wa Kilimanjaro Joyce Ndosi, amesema anawaomba wawekezaji kujitokeza na kuwajengea Kiwanda kikubwa Cha Wanawake wa mkoa huo Ili kuwezesha shughuli za mbalimbali za kijasiriamali kufanyiwa kiwandani hapo.
Ameongeza kuwa zipo ruzuku zinazotolewa kwa Ajili ya shughuli za kijasiriamali lakini kwa mkoa wa Kilimanjaro hawajafanikiwa kupata kutokana na kutofikia vigezo.
Naye Lilian Mosha ,Afisa Jinsia kutoka tasisii isiyokuwa ya kiserikali ya MEEDA inayojishughulisha na maswala ya kilimo, ambayo lengo kubwa ni kuwasaidia wakulima hasa wanawake wanaotoka katika mikoa Isiyopata mvua kwa wingi huku wakijikita katika uzalishaji wa Mazo 7,ambayo ni Alizeti,maziwa,mbogamboga,viungo,mpunga pamoja na mahindi,
Kongamano Hilo limefunguliwa na kaimu katibu Tawala seksheni ya uchumi na uzalishaji Dr Vedast Makota amesema kwa sasa Serikali inayoongozwa na Raisi wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan,imeendelea kuboresha mazingira ya Biashara,kuimarisha diplomasia na nchi nyingine pamoja na kuboresha miundo mbinu Ikiwemo umeme, njia za usafiri,na mawasiliano Ili kuweka mazingira rafiki ya kufanya Biashara.
Kongamano hili limeudhuriwa na Viongozi kutoka tasisii mbalimbali Ikiwemo UTT AMIS,NSSF,SIDO,TRA,TBS NA NEMC.
0 Comments