Header Ads Widget

RC KIGOMA ATAKA MAHAKAMA KUWEKA MAZINGIRA MAZURI YA UPATIKANAJI HAKI

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma


MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amesema kuwa kutokuwepo kwa mazingira mazuri yanayotoa fursa ya upatikanaji wa haki kwa wananchi kunakwanza utekelezaji wa mpango wa maendeleo.


Akizungumza kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre Mjini Kigoma wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria  na kuanza kwa mwaka mpya wa shughuli za mahakama.


Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa kupata haki kwenye mahakama ni haki ya kikatiba ya kila mwananchi mwa mujibu wa ibara ya 17 ya katiba nchi hivyo ni lazima mazingira yawekwe vizuri kuwezesha wananchi kutumia fursa hiyo.


“kukosena kwa mazingira yanayotoa fursa ya wananchi kupata haki ni kikwazo cha maendeleo hivyo uongozi wa mahakama katika ngazi zote na wadau wake wanapaswa kuhakikisha mazingira ya fura ya upatikanaji wa haki kwa wananchi yanakuwa huru na wazi,”Alisema Mkuu huyo wa mkoa.


Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa mazingira ya kupata haki kwa wananchi kwa mkoa Kigoma yametawaliwa na changamoto nyingi ikiwemo uhaba na uchakavu wa majengo ya mahakama, upungufu mkubwa wa watumishi na  uhaba wa vitendea kazi.

Kwa nafasi yake alisema kuwa serikali inachukua hatua katika kutenga bajeti ili kukabiliana na utekelezaji wa wajibu wake wa kuboresha majengo ya mahakama, kuajiri idadi ya kutosha wa watumishi wa sekta ya mahakama na kuhakikisha vifaa na vitendea kazi muhimu vya kuimarisha utendaji haki vinapatikana.


Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa mkoa kuzindua maadhimishi hayo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma alisema kuwa kutokana na kuongeza kwa idadi ya watu na shughuli mbalimbali imefanya pia kuongeza migogoro na mashauri kwenye sekta ya mahakama.



Kutokana na hilo alisema kuwa mahakama ya Tanzania imekuja na mpango wa kutatu migogoro kwa njia ya ushuluhishi  ili kupunguza msongamano wa mashauri mahakamani, mashauri kuchukua muda mfupi kuwezesha shughuli nyingine za kiuchumi ziweze kufanyika.


Jaji Mlacha alisema kuwa Kauli mbiu ya mwaka huu inakuja kukiwa na maboresho makubwa  yanayofanywa na sekta ya mahakama na kutumia usuluhishi kama nyenzo ya kumaliza mashauri ili kuwezesha kuongeza muda wa kufanya kazi badala ya wananchi kutumia muda mwingi kwa ajili ya kuendesha kesi mahakamani.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI