Header Ads Widget

CHAMA CHA MWAPITA KUWAGAWIA VITAMBULISHO WANACHAMA WAKE VITAKAVYOWASAIDIA WAKATI WA KAZI.

 


NA CHAUSIKU SAID

MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.


Chama Cha waendesha pikipiki Mkoa wa Mwanza Chamwapita kimetoa vitambulisho Kwa wananchama wake vitakavyoweza kuwasaidia na kuwatambulisha mahala pa kazi na pindi wanapofikwa na matatizo.


Mwenyekiti wa chama hicho Makoe Kayanda ameeleza kuwa lengo la kutengeneza vitambulisho hivyo na kuvigawa ni kuhakikisha mwanachama anapohitaji msaada wowote kwenye chama au jamii anapata Kwa urahisi Kwa kuwa  wanamtambua.


"Vitambulisho vitawasidia pindi mtu anakiwa amepatwa na tatizo katika kazi zake na kitambulisho hicho kitaweza kumsaidia kupata msaada Kwa kutoa taarifa sehemu husika" Alisema Kayanda.

 

Kayanda ameeleza kuwa Ili mwanachama aweze kupatiwa huduma ni lazima awe na kitambulisho kinachomtambilisha kuwa mwanachama wa chama hicho pamoja na kuwataka waendesha pikipiki na wasio waendesha pikipiki kujiunga kwani chama hicho ni Kwa ajili ya watu wote na sio waendesha boda boda peke yao.




Halima Lutavi ni Afisa Mfawizi Latra ameeleza kuwa vitambulisho hivyo ni  muhimu boda boda hao kuwa navyo kwani vitawasaidia Kwa sehemu kubwa pindi mtu anapofikwa na tatizo hususani kipindi ambacho Yuko nje ya kituo chake Cha kazi.


" Ikitokea mtu amepata tatizo alafu Yuko mbali na kituo chake kulingana na itandawazi uliyopo Kwa sasa anaweza kupata msaada kiurahisi pindi nyaraka zake za kitambulisho zinapoingizwa kwenye mtando Kwa kutumia kitambulisho alichokuwa nacho" Alisema Halima.


Hata vivyo ameeleza kuwa vitambulisho hivyo vitawasidia wao kama Latra kupata takwimu sahihi za waendesha boda boda Mkoa wa Mwanza.


Kwa upande mwingine amewataka waendesha boda boda kukuaa katika maegesho na maeneo ambayo ni salama Kwa kazi zao na kuachana na tabia ya kukaa sehemu ni hatarishi kwao.



" Unakuta mtu amekaa kwenye Kono au chini ya transifoma sehemu ambayo ni hatarishi kwenye maisha yake, ni lazima mjaribu kufikilia nafsi zenu kwanza sio Kila sehemu mnakaa kama hauna sehemu maalumu ya maegesho nenda sehemu husika utapangiwa eneo.


George Masake ni mmoja wa wendesha boda boafa aliyepata kitambulisho ameeleza kuwa vitambulisho hivyo vitawasidia Kwa sehemu kubwa wawapo katika kazi zao, hususani linapotokea tatizo.


"Vitambulisho hivi vitatusaidia Kwa sababu sisi boda boda tunaenda maeneo mbalimbali na sio maeneo ya Mkoa wa Mwanza peke yake Kwa hiyo kuwa na kitambulisho kitasaidia sana.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI