Header Ads Widget

SPIKA WA BUNGE LA INDIA ASIFIA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI



Spika wa bunge la India Mh. Om Birla akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti pamoja na timu ya wabunge kutoka nchi hiyo


Na Pamela Mollel,Matukio Daima Serengeti 

Spika wa Bunge la India Mh.Om Birla ameipokeza Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini  Tanzania kwa kuwa na idadi kubwa ya wanyama wakubwa na rahisi kuonekana ndani hifadhi hiyo


Pia ametaja sababu moja wapo ya yeye kuja Tanzania katika hifadhi hiyo ni ile Filamu ya "The Royal Tour" iliyolenga  kuonyesha vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika Hifadhi zetu hapa Tanzania, ambapo mwigizaji Mkuu alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan 



Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kufanya utalii katika hifadhi hiyo yenye umaarufu mkubwa Duniani alisema kuwa yeye pamoja na timu yake kutoka India wamefurahi sana kuwepo ndani ya Serengeti na wameweza kujionea vivutio mbalimbali kwa ukaribu zaidi


Spika Birla alisema kuwa anaipongeza Tanzania kwa kuwa na vivutio vingi lakini pia Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutangaza utalii wa Tanzania kupitia Filamu ya The Royal Tour 


"Royal Tour imenifanya nitamani sanaa kuja katika hifadhi hii ya Serengeti hakika sehemu hii ni nzurii sanaaa kwa kufanya utalii"alisema Spika Birla 


Aliongeza kuwa yeye pamoja  na timu yake kutoka India wameridhishwa hivyo kuhaidi kuwa mabalozi wazuri wa kutangaza Serengeti katika nchi ya India 


"Tukiwa hapa Serengeti tumejionea wanyama wengi sanaaa wakiwemo Simba ,Twiga,Faru,nyumbu na wengine wengi"alisema Spika Birla 


Naye Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama ya Bunge Vita Rashid kawawa alisema Spika wa India alipewa mwaliko na Spika wa bunge la Tanzania kama Diplomasia ya kibunge baina ya Tanzania na India 


"Leo wameweza kupata picha kuwa Serengeti ni mahali pakuja na kuweza kuonana wanyama wakubwa  tena kirahisi zaidi na wakitoka hapa wataweza kututangazia hifadhi na kupitia fursa hiyo tutapata watalii wengi kutoka India"alisema Kawawa


Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Uhifadhi Herman Batiho anayesimamia Uhifadhi na maendeleo ya Biashara alisema wao kama shirika la hifadhi za Taifa Tanapa wamefarijika kupata ugeni huo wenye jumla ya watu 12 wakiongozwa na Spika wa Bunge la India 


Alisema kuwa wanatarajia kupata idadi kubwa ya watali kutoka India kuja Tanzania kufanya utalii kutoka na Spika huyo pamoja na wabunge walioambatana nao kuhaidi kuwa mabalozi wazuri wa kutangaza hifadhi ya Taifa Serengeti 


"Taifa la India linasifika kwa kuwa na watu wengi zaidi hivyo tunategemea kupata watalii wengi na ugeni huu umefurahi sana kuwepo katika hifadhi hii"alisema Batiho Kushoto Prosper Minja

Afisa Habari Mwandamizi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ni Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje,ulinzi na usalama ya Bunge Vita Rashid Kawawa,kulia ni Mhifadhi kutoka Shirika la hifadhi za Taifa Tanapa Mohammed Kiganja wakiteta jambo ndani ya hifadhi ya Serengeti

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI