NA GIFT MONGI,MATUKIO DAIMA APP MOSHI.
Mbunge wa jiimbo la Vunjo Dkt Charles Kimei amehakikishia wanavunjo kuwa ilani ya uchaguzi 2020-2025 itaenda kuwa ya kihistoria kutokana na miradi ya kimkakati inayotekelezwa Kwa sasa.
Dkt Kimei alitoa kauli hiyo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM jimbo la Vunjo 2021-2022 yenye thamani ya zaidi ya Tshs 10 bilioni ambapo ndani yake ipo miradi ambayo tayari imeshakamilika na mingine ipo mbioni kukamilika.
Katika uwasilishwaji huo aliwashukuru wananchi wote wa jimbo la Vunjo kwa ushirikiano mkubwa wanaompatia katika kutekeleza majukumu yake ya uwakilishi.
"Nawashukuru viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilaya na mkoa, wanachama wote wa CCM pamoja na watendaji wa serikali wakiongozwa na mkuu wa mkoa Kilimanjaro na wilaya ya Moshi kwa ushirikiano wao wanaompatia"alisema
Pia mbunge amewahakikishia wananchi wa jimbo la Vunjo kuwa ataendelea kusimamia maslahi mapana ya wananchi wa jimbo la Vunjo katika ustawi wa maendeleo.
Katika hatua nyingine Dkt Kimei amenunua miche ya parachichi aina ya HASS yenye thamani ya zaidi ya shilingi million 7.5 kwa ajili ya kuwapatia wananchi kwa kuanzia huku malengo ni kuendelea kusambaza miche hiyo bora kutoka wizara ya Kilimo kupitia taasisi yake ya wakala wa mbegu za Kilimo (ASA).
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi alimpongeza Dkt Kimei kwa ufatialiaji mzuri wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika jimbo la Vunjo, ambapo pia amemhakikishia kuwa Chama kinatambua jitihada zote zinazofanywa.
"Mwenye macho haambiwi tazama tunashukuru kwa namna unavyoisimamia ilani lakini pia kuhakikisha mandeleo yanakuja kwa wananchi hakika hili ni jambo la kuigwa"alisema
0 Comments