Header Ads Widget

KONGAMANO LA WADAU WA MAENDELEO VUNJO LAAHIRISHWA... NI KUFUATIA AJALI ILIYOSABABISHA VIFO VYA WATU WATANO

 

Na Gift Mongi MATUKIO DAIMA APP MOSHI.

Kongamano la wadau wa maendeleo katika jimbo la Vunjo lililopo Moshi mkoani Kilimanjaro lililotarajiwa kufanyika Dec 20 limeahirishwa kutokana na ajali ya kuporomoka kwa  ghorofa iliyosababisha vifo vya watu watano.


Taarifa kutoka ofisi ya mbunge wa Vunjo Dkt Charles Kimei imeelezwa kusikitishwa na tukio hilo ambalo limeacha simanzi katika kaya kadhaa baada ya kuondokewa na wapendwa wao


"Nawapa pole kwa wale waliopatwa na msiba au kuguswa na tukio hili lakini pia Kwa wanavunjo wote Mungu awape moto wa subira katika kipindi hiki kigumu"imeelezwa


Hata hivyo mbunge huyo tayari alikuwa amendaa kongamano hilo ambalo lingewakutanisha wadau mbali mbali ili kuweza kubadilishana mawazo na kuona njia sahihi za kuleta maendeleo kwa wananchi mwaka ujao.


Kamanda wa Polisi Kilimanjaro Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema jengo hilo lilikuwa linajengwa na mafundi walikuwepo jumla ya watu thelathini .


"Jengo hilo lilikuwa linajengwa na wafanyakazi walikuwa 30, wafanyakazi 5 wamefariki na 9 kujeruhiwa na wanapatiwa mtibabu,marehemu mmoja bado haja fahamika hivyo wananchi wanapaswa kwenda kutambua mwili huo,bado jengo hilo linafukuliwa zaidi"amesema


Kwa mujibu wa kamanda Maigwa ni kuwa watu wote waliopoteza maisha ni wanaume ambao ndio walikuwa mafundi katika jengo hilo la ghorofa mbili


Mkuu wa wilaya ya Moshi Abbasy Kayanda ambaye pia ni kaimu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro amesema kwa sasa kamati inaenda kuundwa ilu kuweza kubaini chanzo cha ajali hiyo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI