NA HADIJA OMARY LINDI
.....ZAIDI ya vijana Elfu 4,000 kutoka Mikoa ya Lindi, Manyara , Dodoma , kipawa Dar es salaam kunufaika na Mafunzo katika vyuo vya VETA kupitia program ya Ajira na ujuzi kwa maendeleo ya Afrika (E4D) utakaoghalimu kiasi cha shilingi bilioni 1.32 .
Hayo yameelezwa na kiongozi wa mradi wa program ya (E4D) , ajira na ujuzi kwa maendeleo Barani Afrika, Kabogo Mbuyi wakati wa ghafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya mafunzo kwa wizara ya Elimu , sayansi na Teknolojia yaliyofanyika katika Chuo cha ufundi Stadi VETA Mkoani Lindi yaliyoenda sambamba na utiaji saini makubaliano kati ya shirika la maendeleo la Ujerumani GIZ na mamlaka ya Elimu na mafunzo ya ufundi Stadi VETA.
Mbuyi alisema program hiyo ya E4D inalenga kukuza ajira endelevu na kuboresha hali za ajira kupitia ushirikiano mpana wa sekta za umma na binafsi hasa katika kukuza ajira katika sekta za ujenzi na matengenezo , nishati mbadala pamoja na utalii
Alisema Nchini Tanzania mpango huo unatekelezwa kupitia shirika la maendeleo la Ujerumani (GIZ) pamoja na ofisi ya Waziri Mkuu, kazi, Vijana, Ajira, na watu wenye ulemavu ambao kwa awamu ya kwanza utatekelezwa mpaka mwezi Desemba mwaka 2023.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzj Mkuu wa VETA Felix Staki alisema mradi wa ajira na ujuzi kwa vijana barani Afrika (E4D) ndani ya VETA unatarajiwa kutekelezwa katika vyuo vinne ambavyo ni VETA Lindi, VETA Kipawa , VETA Dodoma na VETA Manyara ukihusisha mafunzo ya muda mfupi, mafunzo kwa walimu na ununuzi wa vifaa
Alizitaja Fani zinazotarajiwa kutolewa ni pamoja na ufundi bomba majumbani na viwandani, Uchomeleaji na uungaji vyuma na Mechotronics.
Staki aliongeza kuwa katika chuo cha VETA Lindi mradi huo umetoa vifaa vyenye thamani ya shilingi 228, 571, 000/= kwa ajili ya fani za ufundi bomba , uchomeleaji na uungaji vyuma ambapo wanafunzi 700 wanatarajiwa kunufaika kwa kupatiwa mafunzo ya muda mfupi.
Alisema kuwa utekelezaji wa Mradi huo wa E4D katika chuo cha VETA Lindi na vyuo vingine utachangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza udahili, kutoa fursa zaidi kwa vijana kupata ujuzi kupitia mafunzo ya ufundi stadi, kuimarisha ubora wa mafunzo ya ufundi stadi kwa kuwa chuo kimepata vifaa vya kisasa vya kufundishia pamoja na kuongeza ujuzi kwa walimu wq ufundi stadi kupitia kipengele cha TOT.
Naye Mkuu wa Chuo cha ufundi Stadi VETA Mkoani Lindi Eng. Harry Mmari alitumia fursa hiyo kuwashukuru wadau wa maendeleo GIZ Pamoja na shirika la ushirikiano wa kimataifa la korea (KOICA) kwa msaada huo wa vifaa ambavyo vitasaidia kutoa mafunzo na kutengeneza Ajira kwa vijana .
Mmari alishukuru pia kwa kuanzisha fani ya mabomba kwa kuwa walikuwa wana ihitaji sana katika chuo hiko na kwamba kutokana na umuhimu wa fani hiyo alimuomba kaimu mkurugenzi kuwapatia usajiri wa kozi ndefu ili waweze kuwa na uwanda mpana zaidi wa kufundisha vija a na hatimae kupata mafundi wengi wa fani hiyo.
Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainab Telack alisema kuwa kupitia program hiyo ni matarajio ya Serikali ya Mkoa huo kuona watoto watakaomaliza mafunzo hayo watakuwa na ujuzi wa kutosha utakaowawezesha kushindana kwenye soko la ajira na vijana wanaotoka kwenye vyuo vingine.
"VETA sasa inashindana na vyuo vingine ambavyo vinatoa ujuzi kwa Elimu ya kati , vyuo kama Mbeya Technique, Arusha Technique na vyuo vingine, watoto wetu wanaotoka hapa wapate ujuzi ambao watakwenda kushindana na wanafunzi hao kwenye soko la Ajira "
"Ninaamini kwa vifaa ambavyo nimeviona inawezekata kwenye vyuo vingine vya kati pia vifaa hivi havipo, hiyo ni fursa kubwa ambayo watoto wetu wa VETA ambayo wameipata na niwaombe wanafunzi tumieni fursa na vifaa hivyo kujifunza kwa kujipa muda wa kutosha kusoma ili muweze kupata ujuzi unaofaa " alieleza Telack
0 Comments