Header Ads Widget

MELI YA KITALII YA ZAANDAM YATIA NANGA BANDARI YA DAR ES SALAAM

 


Meli ya Kitalii ya Zaandam kutoka Florida, Marekani imetia nanga Katika Bandari ya Dar es Salaam ikitokea nchini Misri ikiwa katika ziara yake ya siku 71, kutembelea Nchi mbalimbali Barani Afrika na vivutio vya Utalii Katika Nchi hizo.


Meli hiyo ambayo ni moja kati ya Meli kubwa za Watalii, imetia nanga ikiwa na Watalii 1060 kutoka Mataifa ya Marekani na Ulaya pamoja na Wafanyakazi wa Meli 520 kutoka Mataifa 35 Duniani.


Meli hiyo imepokelewa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Mathew Anthony, ambaye amesema ujio wa Watalii hao ni sehemu ya zao la Utalii hapa nchini kupitia Filamu ya Royal Tour


Watalii hao watakuwa nchini kwa siku Nne ambapo Novemba 10 na  Novemba 11, 2022 watafanya Utalii Katika Jiji la Dar es Salaam, mji wa kale wa Bagamoyo na Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na Novemba 12 na Novemba 13, 2022 watatembelea Visiwa vya Zanzibar.


Baada ya kutoka Zanzibar, Meli hiyo ya Watalii itaendelea na Safari yake kwa kutembelea nchi za Madagascar, Afrika kusini, Msumbiji, Namibia na nchi nyingine za Afrika.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI