Header Ads Widget

WARATIBU WA AFUA ZA VVU, UKIMWI NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA MAHALA PA KAZI WATAKIWA KUTENGA BAJETI KWA AJILI YA AFUA ZA VVU , UKIMWI NA MSY

 


NA HADIJA OMARY, LINDI

KUELEKEA  Maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani Desemba 1 ambayo kitaifa yanatarajiwa kufanyika Mkoani Lindi waratibu wa afua za virusi vya ukimwi VVU, UKIMWI na magonjwa sugu  yasiyoambukiza MSY kutoka ngazi ya wizara leo wamekutana na kufanya kikao cha pamoja na   kamati ya kitaifa ya kudhibiti  magonjwa hayo mahali pakazi.


Akizungumza katika kikao hiko Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Xavier Daudi , alisema kuwa madhumuni ya kikao hiko ni kupokea taarifa za utekelezaji wa miongozo ya Serikali kutoka katika mikoa husika na taarifa katika ngazi ya wizara na kupeana ushauri wa namna bora ya kuimarisha uratibu wa afua za virusi vya ukimwi (VVU)  ukosefu wa kinga mwilini (UKIMWI) na magonjwa yasiyoambukiza (MSY) katika Ngazi mbali mbali ili kufikia malengo ya kitaifa na kimataifa kuhusu udhibiti wa VVU na UKIMWI nchini.


Hata hivyo aliwataka waratibu kuhakikisha wanatenga Bajeti kwa kuzingatia utekelezaji wa nyaraka zote zilizoainisha katika mwongozo na waraka wa kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa yasiyoambukiza (MSY) 2014 pamoja na utoaji wa huduma kwa watumishi waliojiweka wazi, mafunzo kwa kamati, waelimisha rika na watumishi.


Aidha pamoja na mambo mengine aliwataka waratibu hao kuongeza ubunifu ili kuwashawishi watumishi wanaoishi na VVU na UKIMWI kujiweka wazi ili waweze kuhudumiwa kwa mujibu wa miongozo iliyopo na hatimaye kutekeleza malengo ya kimataifa ya 95 tatu na 0 (sifuri ) tatu.


Kwa upande  wake msimamizi wa kinga ya virusi vya ukimwi ngazi ya Taifa , tume ya udhibiti ukimwi Tanzania , DR. Hafidh ameir  Alisema kuwa kikao hiko ni cha kawaida ambacho kinawakutanisha  waratibu wa VVU, UKIMWI na magonjwa sugu yasiyoambukiza (MSY) mahala pakazi kutoka ngazi ya wizara kila robo mwaka ambapo ufanyika katika mikoa mbali mbali  kwa kukutana na kamati za ngazi ya mkoa  lengo likiwa ni kueleza shughuli mbali mbali za afua za Virusi vya ukimwi (VVU) UKIMWI na magonjwa yasiyoambukiza mahala pa kazi.


Alisema  Tanzania ni kama Nchi zingine ulimwenguni ambazo zinatekeleza malengo ya kitaifa na kimataifa katika jitihada za kutokomeza na kudhibiti maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) , Ukosefu wa kinga Mwilini ( UKIMWI) ili kufikia 95, 95, 95 ifikapo 2025 na sifuri 3 ifikapo 2030


“ Tanzania inalenga kuhakikisha inafikia lengo la kitaifa la 95, 95, 95 kwa maana ifikapo 2025 asilimia 95 ya wanaoishi na virusi vya ukimwi (VVU) wanatambua hali zao, asilimia 95  ya WAVIU wawe wameanza dawa za kupunguza makali ya VVU na asilimia 95 ya mwisho ya walioanza dawa wapunguze kiwango cha virusi mwilini” alisema.


“madhumuni makubwa ni kufikia malengo ya kitaifa ambapo kwa mwaka 2030 tunapaswa kufikia sifuri 3 tukilenga kufikia mwaka huo kusiwepo na maambukizi mapya , kusiwepo unyanyapaa na kusiwepo na vifo vitokanavyo na ukimwi”


Kwa upande wake mkurugenzi msaidizi wa sehemu za anuwai za jamii ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mwanaamani Juma alisema vikao hivyo vya kitaifa vinalengo la kuhakikisha wanaongeza usimamizi na utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI katika maeneo ya pembezoni sambamba na kutoa ushauri na namna nzuri ya utekelezaji kwa Taasisi za Utumishi wa Umma na hatimaye  kuzijengea uwezo utakaowawezesha kutekeleza afua hizo ili Taifa liweze kuwa na watumishi wa Umma wenye Afya.


Alisema sehemu za anuwai za jamii katika utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa Umma na utawala bora pamoja na majukumu mengine pia ina jukumu la kushughulikia  afua za VVU, UKIMWI na magonjwa sugu yasiyoambukiza (MSY) mahala pakazi katika utumishi wa Umma .


Awali akitoa Taarifa ya kudhibiti VVU/UKIMWI na Magonjwa sugu yasiyoambukizwa mahala pa kazi katika utumishi wa Umma kwa Mkoa wa Lindi, katibu Tawala wa Mkoa huo Ngusa Samike alisema mkoa huo unaendelea kutekeleza mwongozo wa kudhibiti maambukizi ya VVU/UKIMWI na magonjwa yasiyoambukizwa mahala pa kazi ambapo utekelezaji wake unafanyika kwa halmashauri zote sita kwa kufuata mwongozo uliotolewa februari 2014.


Samika pia alisema Mkoa huo una jumla ya watumishi 8,630 kati yao watumishi 113 wanaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi, watumishi 108 kutoka mamlaka za mitaa na watumishi 5 kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa na watumishi 500 wana magonjwa sugu yasiyoambukiza ambapo wananufaika na utekelezaji wa mwongozo.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI