Header Ads Widget

PWANI WASALIMISHA SILAHA 111


KUFUATIA tangazo lililotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni Agosti 26 mwaka huu kutaka silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria kusalimishwa jumla ya silaha mbalimbali 111 zimesalimishwa mkoani Pwani.


Zoezi hilo ambalo lilianza Septemba Mosi hadi  Oktoba 31  mwaka huu ambapo watakaosalimisha ndani ya muda uliopangwa hawatachukuliwa hatua za kisheria na baada ya hapo watakaokutwa na silaha kinyume cha taratibu watachukuliwa hatua za kisheria. 


Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani ACP Pius Lutumo alisema kuwa mafanikio ya kupatikana silaha hizo ni makubwa baada ya wananchi kuelimishwa.


Lutumo alisema kuwa silaha zilizosalimishwa ni gobore 101, short gun saba, rifle mbili na bastola moja ndizo zilizo salimishwa katika muda uliopangwa.


Alitaja Wilaya zilizosalimisha silaha kuwa ni Chalinze silaha 72, Mlandizi silaha 19, Bagamoyo silaha 13, Kisarawe silaha 4 na Kibaha 3.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI