Mamlaka ya
kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) inawashikilia watu 11 kwa
tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya miongoni mwao akiwa ni Kocha wa Makipa wa
Simba sc Muharami Mohamed maarufu kama ‘Shilton’.
Hayo
yameelezwa leo Novemba 15, 2022 na Kamishna Jenerali wa DCEA, Gerald Kusaya
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mamlaka hiyo imesema iliendesha Operesheni
katika maeneo mbali mbali nchini na kukamata Jumla ya Kilo 34.89 za dawa za
kulevya aina heroin pamoja na kukamata biscuit 50 zilizotengenezwa kwa kutumia
dawa za kulevya aina ya Bangi kama moja ya Malighafi.
Mtuhumiwa
mwingine miongoni mwa hao waliokamatwa ni Kambi Zubeir Seif ambaye ni Mfanyabishara
na Mmiliki wa Kituo cha Michezo cha Cambiasso kilichopo Tuangoma, Kigamboni Dar
es Salaam na pia ni mmiliki wa Kampuni ya Safia Group of Companies ambayo ina
miliki magari ya kusafirisha abiria (daladala) kutoka jijini Dar es salaam
Kwenda mkoa wa Pwani, na Said Matwiko mkazi Magole jijini Dar es salaam.
0 Comments