Header Ads Widget

CCM YAPATA MWENYEKITI MPYA


 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kimemchagua  Mwishehe Mlao kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho.


Mlao alishinda baada ya uchaguzi huo kurudiwa  na kupata kura 479 dhidi ya Farida Mgomi aliyepata kura 341.


Uchaguzi huo ulirudiwa baada ya wagombea wa nafasi hiyo kutopata nusu ya kura zilizopigwa ambapo hatua ya kwanza Mlao alipata kura 392 huku Mgomi akipata kura 361.


Akimtangaza mshindi wa nafasi hiyo kwenye uchaguzi huo ambao ulifanyika Kwa Mathias Mjini Kibaha msimamizi akiwa ni Zainabu Telaki alimtangaza Mlao kuwa mshindi.


Kura za awali zilizopigwa zilikuwa 841 zilizoharibika zilikuwa 8 halali  hivyo kura halali kuwa ni 833 ambapo Mwishehe Mlao alipata kura 392 akifuatiwa na Farida Mgomi 367 Imani Madega alipata kura 61 na wa mwisho alikuwa ni  Shaibu Mtawa aliyepata kura 13 


Uchaguzi huo ulirudiwa kwa kuwakutanisha wawili hao ambapo waliopiga kura walikuwa 824 kura zilizoharibika zilikuwa 4 na kura halali zikiwa 820 Mwishehe Mlao alipata kura 479 Farida Mgomi alipata kura 341.


Mlao akishikuru wajumbe alisema kuwa uongozi wake utakuwa shirikishi ili kuleta mafanikio ya chama na Maendeleo kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI