Header Ads Widget

MAMA AUA WATOTO WAKE WAWILI KWA SUMU-KIGOMA

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma Filemon Makungu ACP akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake tukio la mauaji ya watoto kunyweshwa sumu na mama yao mzazi

                                                                            XXXXXXXXXXX

Na Editha Karlo, Kigoma

WATOTO wawili wameuawa na mama yao mzazi baada ya kuwapa sumu huku mmoja akinusurika kifo.


Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma Filemon Makunga ACP alisema kuwa tarehe 20 mwezi huu majira ya saa tatu usiku katika mtaa wa shede,Manispaa ya Kigoma Ujiji kulitokea tukio la vifo vya watoto wawili baada ya kunyweshwa sumu.


Kamanda Makungu alisema kuwa watoto hao walinyweshwa dawa inayodhaniwa kuwa ni aina ya Tiktik ya kuoshea mifugo kitendo ambacho ni kinyume na sheria za ukiukwaji wa haki za binadamu.


Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Bi. Christina Akoonay(36) ambaye ni mama mzazi wa watoto hao waliofariki alikutwa akiwa amejifungia ndani ya nyumba anayoishi akiwa na watoto wake hawajitambui baada ya kunywa sumu.


Aliongeza kwa kusema kuwa mama huyo na watoto wake walikimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma(Maweni)kwa ajili ya kupatiwa matibabu,baada ya kufanyika uchunguzi ilibainika kuwa wamekunywa sumu,wakati wakiendelea na matibabu mtoto mwingine alifariki dunia.


Alisema mtoto mmoja bado amelazwa na mama yake wakiendelea na matibabu japo hali zao sio nzuri,Jeshi la polisi wanaendelea na Uchunguzi wa tukio hilo.


Naye mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mkoa wa Kigoma Dkt Stanley Binagi amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema watoto hao wanasadikiwa kupewa sumu ambayo ni dawa ya kuua wadudu kwenye mifugo na mimea.


Alisema mama huyo alikunywa sumu hiyo akiwa ni mjamzito ambapo mpaka sasa sumu haijaweza kuathiri mtoto aliyeko tumboni japo mama huyo alizimia kwa muda mrefu wakati yupo hospitalini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI