Header Ads Widget

DR.BASHIRU AZIDI KUSHAMBULIWA, NJOMBE NAKO WAMUWASHIA MOTO


 

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Makundi mbalimbali ya wanasiasa na wanazuoni mkoani Njombe wamekosoa na wengine kupongeza kauli za mbunge wa kuteuliwa Dokta Bashiru Ally akiwa mkoani Morogoro aliyewataka wakulima kuacha tabia ya kusifia viongozi kwa kutekeleza wajibu wao  kupitia mtandao wa vikundi vya wakulima wadogo MVIWATA.


Mjadala huo umevuta hisia za watanzania wengi wakiwemo wabunge na viongozi mbalimbali ambapo sehemu ya hotuba yake na wakulima kupitia mkutano wao wa  MVIWATA Dokta Bashiru alisema mtandao huo haupaswi kuwa sehemu ya kusifu utendaji kazi wa viongozi na badala yake wajitetee wenyewe.



Wakizungumza na vyombo vya habari wadau hao akiwemo mwanazuoni  Iman Fute ambaye ni diwani wa kata ya Kitandililo mjini Makambako amesema Dr.Bashiru alishindwa kutambua ni sehemu gani ya kutolea maoni yake ilihali anafahamu utaratibu wote wa chama Cha mapinduzi huku Mhadhiri wa chuo kikuu Cha Tumain Iringa Dr.Lechion Kimilike  akimpongeza Bashiru kwa kuwatetea wakulima.


Mzee Lukule Mponji mwenyekiti wa TLP mkoa wa Njombe naye anasema Dokta Bashiru Ally alitekeleza wajibu wake wa kuwatetea wakulima ambao wamekuwa hawana jukwaa la kuwasemea changamoto zao.



Venance Ngimbudzi ni mwenyekiti mstaafu wa mtandao wa vikundi vya  wakulima MVIWATA mikoa ya Njombe na Iringa ambaye anasema kauli ya Dkt.Bashiru ni malalamiko ya wakulima wenyewe hivyo hapaswi kushambuliwa mitandaoni bila kufuatilia jambo lilivyo.


Mbunge wa jimbo la Lupembe Edwin Enosy Swalle yeye anasema Dokta Bashiru hakupaswa kuzungumza maneno hayo akiwa kiongozi dhidi ya viongozi wa serikali na kuzuia pongezi kwa mazuri yanayofanywa.


Viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani wanasifu kauli ya Dokta Bashiru huku wengine wakipinga vikali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI